Mkoa wa Mwanza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mkoa wa Mwanza
Mahali pa Mkoa wa Mwanza katika Tanzania
Mahali pa Mkoa wa Mwanza katika Tanzania
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.75°S 32.75°E / -2.75; 32.75
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Mwanza
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Abas Kandoro
Eneo
 - Mkoa 19,592 km²
Idadi ya wakazi (2002)
 - 2,942,148
Tovuti: http://www.mwanza.go.tz/
Mwanza

Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, wenye postikodi namba 33000. Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.

Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2. Wilaya ndizo Ukerewe, Magu, Sengerema, Geita, Misungwi, Kwimba, Nyamaganga na Ilemela. Jiji la Mwanza lina ndani yake wilaya za Nyamagana na Ilemela.

Ramani (kabla ya 2012) Wilaya au manisipaa Wakazi (2002) Tarafa Kata Kijiji Eneo km²
Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Wilaya ya Geita 712,195
Wilaya ya Ilemela 265,911
Wilaya ya Kwimba 316,180
Wilaya ya Magu 416,113
Wilaya ya Misungwi 257,155
Wilaya ya Nyamagana 210,735
Wilaya ya Sengerema 501,915
Wilaya ya Ukerewe 261,944
Jumla 2,942,148 19,592
Mkoa wa Mwanza una Halmashauri za Wilaya tatu sita ambazo ni Geita, Sengerema, Magu, Misungwi,
Kwimba na Ukerewe na Halmashauri ya Jiji la Mwanza inayohudumia wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Marejeo: Mkoa wa Mwanza

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Makabila makubwa ya Mwanza ndio Wasukuma upande wa bara, halafu Wakerewe na Wakara visiwani.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Mwanza

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]