Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Njombe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa mpya wa Njombe umechukua eneo lote la kusini la Mkoa wa Iringa katika Tanzania. Rangi iliyokolea inaonyesha wilaya ya Njombe tu kabla haijagawanywa.
Wilaya za Mkoa wa Iringa na mikoa jirani hadi mwaka 2010.

Mkoa wa Njombe ni mmojawapo kati ya mikoa mipya nchini Tanzania wenye postikodi namba 59000 , ukiwa umeanzishwa rasmi mwaka 2012[1]. Umepakana na mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Mbeya na Iringa.

Kutokana na hadhi mpya, wilaya ya Njombe imegawanyika kati ya ile ya mjini na ile ya vijijini. Pia, mwezi wa Machi 2012, imeanzishwa wilaya ya Wanging'ombe.

Mkoa una wakazi 889,946 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [2], ukishika nafasi ya mwisho kati ya mikoa ya Tanzania Bara. Mchanganuo katika wilaya zake sita ni kwama ifuatavyo: Njombe Mjini (wakazi 182,127), Njombe Vijijini (wakazi 109,311), Makambako (wakazi 146,481), Makete (wakazi 109,160), Ludewa (wakazi 151,361), Wanging'ombe (wakazi 191,506).

Mwaka 2012 katika eneo hilo kulikuwa na wakazi 702,097 [3] katika wilaya sita zifuatazo: Njombe Mjini (wakazi 130,233), Njombe Vijijini (wakazi 85,747), Makambako (wakazi 93,827), Makete (wakazi 97,266), Ludewa (wakazi 133,218), Wanging'ombe (wakazi 161,816).

Makao makuu yako Njombe mjini.

Makabila makubwa ya wenyeji mkoani Njombe ni Wabena, Wakinga na Wapangwa, na uwiano wao ni 37:11:3.

Kabila la Wabena liko wilaya ya Njombe na eneo la Malangali likiwa linapakana na wilaya ya Ulanga na wilaya ya Mlimba (Mkoa wa Morogoro), Wakinga wako wilaya ya Makete na Wapangwa wako katika wilaya ya Ludewa.

Yapo pia makabila madogo kama vile Wawanji, Wakisi, Wamanda, Wamagoma n.k. ambao kwa ujumla wao wanachukua asilimia 6 iliyosalia ya watu mkoani.

Karibu wakazi wote wa mkoa ni Wakristo, hasa Walutheri na Wakatoliki.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Staff. "Tanzania: State Gazettes New Regions, Districts", 9 March 2012. Archived from the original on August 23, 2012. 
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. "Census 2012". National Bureau of Statistics. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 5, 2016. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2016. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Njombe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.