Mkoa wa Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa Taifa
Mahali pa Mkoa wa Dar es Salaam katika Tanzania.
Dar es Salaam miaka ya 1930.
Machweo jijini
Ghorofa ndefu kuliko zote za Afrika Mashariki.
Makao makuu ya Benki kuu ya Tanzania.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Shamba la Mungu.

Dar es Salaam ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Mkoa wa Pwani pande zote barani na Bahari ya Hindi upande wa mashariki.

Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 5,383,728[1].

Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.

Majimbo ya bunge[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


  1. https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/