Nenda kwa yaliyomo

Kitila Mkumbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kitila Alexander Mkumbo ni mwanasiasa wa CCM wa Tanzania na mbunge anayewakilisha jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, tangu mwaka 2020.[1]

Kitaaluma ni profesa kutoka kitivo cha elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alikuwa Waziri wa Uwekezaji chini ya ofisi ya Rais, kwa sasa kama Viwanda na Biashara.[2]

Wakati wa uongozi wa John Magufuli, rais alimteua Mkumbo kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.[3]

Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimteua kama Waziri wa Viwanda na Biashara katika baraza lake la mawaziri la awali. Hata hivyo, kuanzia Julai 2023 hadi sasa, anahudumu kama Waziri katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, baada ya mabadiliko kadhaa ya wizara. [4]

Kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje.[5]

  1. "Bunge Polis". www.parliament.go.tz. Iliwekwa mnamo 2021-07-24.
  2. "Prof Kitila Mkumbo". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-07-24.
  3. "Prof. Kitila Mkumbo Profile under Ministry of Water and Irrigation" (PDF).
  4. https://www.eatv.tv/news/current-affairs/rais-samia-awateua-tena-mwigulu-na-profesa-kitila
  5. https://www.epza.go.tz/index.php/administration/board-members/33