Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Dar es Salaam
Jiji la Dar es Salaam kama linavyoonekana kutoka Mafuta House
Jiji la Dar es Salaam kama linavyoonekana kutoka Mafuta House

Nembo
Dar es Salaam is located in Tanzania
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Lokeshen Dar es Salaam
Anwani ya kijiografia: 6°48′0″S 39°17′0″E / 6.8°S 39.28333°E / -6.8; 39.28333
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Idadi ya wakazi (2012)
 - 4,364,541

Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Pia ni jina la Mkoa wa Dar es Salaam. Dar es Salaam ni mji mkongwe na wenye mamilioni ya watu katika nchi ya Tanzania. Dar es Salaam ndio mji wenye vitega uchumi vingi na ndio mji unaoangaliwa.

Ni mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania wakati Dodoma ni makao makuu ya Tanzania tangu mwaka 1973. Mpango wa kuhamishia serikali mjini Dodoma bado unaendelea, japokuwa bado ofisi nyingi za serikali, ikiwa ni pamoja na Ikulu, zipo Dar es Saalaam.

Mji una wakazi wapatao 4,364,541 kwa hesabu ya sensa iliyofanyika katika mwaka wa 2012.[1]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jiji hili zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.

Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu mwaka 1904 viliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara ya leo kuwa eneo lindwa la Tanganyika chini ya Uingereza.

Sanamu ya askari mjini Dar es Salaam

Wakazi na uchumi[hariri | hariri chanzo]

Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ofisi kuu za viongozi wa serikali, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k.

Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k.

Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika wilaya za Temeke, Ilala, na Kinondoni.

Wakazi na uchumi[hariri | hariri chanzo]

Dare es salaam ni mji unaosemekana kuwa mkubwa kuliko yote kwa sababu ya maendeleo mbalimbali ya viwanda;uwepo wa bahari;uwepo wa sehemu mbalimbali za kihistorian.k.

Huduma za Jiji[hariri | hariri chanzo]

Huduma ya maji Dar es Salaam imekuwa na tatizo kubwa katika kudhibiti mfumo wa maji taka katika mkoa wa Dar es Salaam kwa muda mrefu. Tangu shirika la maji DAWASCO (Dar es Salaam Water Supply Company) lilipowekwa rasmi kama shirika husika katika kuratibu utaratibu mzima wa mfumo wa maji safi na maji taka, kumekuwa na nafuu kidogo tu, lakini baada ya muda, liliibuka tatizo la kuibiwa kwa mabomba na uharibifu wa vyanzo mbalimbali vya maji.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Kwenye suala hili la elimu vijana wanatakiwa kupewa elimu; hasa vijana wa mitaani wasioingiza kipato inabidi wapewe elimu kwa kazi fulani ili waweze kuajiriwa na kulipa faida taifa kwa kuingizia kipato na kukuza uchumi wa taifa. Mfano wa kazi hizo ni kama ujenzi wa nyumba n.k.

Picha za Dar es Salaam[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: