Kurani
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Kurani (kwa Kiarabu: القرآن, Qur'an) ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinatazamwa na Waislamu kama "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hiki kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya vitabu vya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.
Lugha na tafsiri[hariri | hariri chanzo]
Imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,400.
Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake"
Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran tukufu na Waislam, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu.
Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile siyo ya Qur'an tukufu na wala siyo ya kweli; ni kopi ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli.[1]
Historia[hariri | hariri chanzo]
Waislamu wanaamini kwamba Qur'an tukufu mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti wake ilipomfikia.
Qur'an tukufu haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani.
Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Qur'an na kuwa kitabu kitakatifu.
Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Qur'an tukufu.
Elementi, Sura, Mistari, Aya[hariri | hariri chanzo]
Kuna sehemu 30 katika Qur'an, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari.
Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina.
Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Ma'ida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Ra'd, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan.
Mahusiano baina Qur'an na Biblia[hariri | hariri chanzo]
Katika Qu'ran tukufu, inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizi pamoja na Uislamu huitwa za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano haya.
Kuna baadhi ya kurasa za Qu'ran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Qu'ran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abraham, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Yobu, Zakaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu.
Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Qu'ran tukufu inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu.
Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Qu'ran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo.
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Qur'an, Encyclopedia Britannica, retrieved on 8 Januari 2009
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Al-Quran (Qurani) online kwa Kiarabu na tafsiri zaidi ya 100 katika lugha 20 pamoja na Kiswahili
- Quran.com
- Swahili Quran Tasfir by Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, tarjuma ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani inapatikana hapa , tovuti ya archive.org
- Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
- QUR,ANI TUKUFU na tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili Quran Kareem.
![]() |
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kurani kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |