Zaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Zaka (kutoka neno la Kiarabu زكاة, zakat, lenye maana ya "kinachotakasa") ni toleo la sehemu ya mapato ambalo muumini wa dini fulani anapaswa kutoa.

Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Desturi ya Mashariki ya Kati ya kutoa sehemu moja ya kumi kwa makuhani iliingia katika Uyahudi kuanzia Abrahamu aliyempa Melkisedek mfalme wa Salem aliyekuwa pia kuhani wa El Elyon (Mungu Mkuu).

Habari hiyo inasimuliwa katika Kitabu cha Mwanzo 14:18-20 na kusisitizwa na Waraka kwa Waebrania 7:5.

Zaka (kwa Kiebrania מעשׂר, ma‛ăśêr, kwa Kigiriki δεκάτη, dekatē) inaagizwa na vitabu vingine vya Biblia ya Kiebrania, kama vile Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Sheria katika Torati.

Baadaye wajibu huo ulisisitizwa na Kitabu cha Malaki 3:8-12 na Kitabu cha Tobiti 1:6–8.

Katika Agano Jipya, mtume Paulo alifundisha kuwa anayetumikia kwenye altare anastahili kupata riziki zake kwa njia hiyo (Waraka wa kwanza kwa Wakorintho 9:13).

Katika Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Stoo ya zaka huko Kronenburg, Ujerumani.

Mwanzoni mwa Kanisa waamini walikuwa wanawajibika, lakini baadaye zilianza kutolewa sheria ili kuwahimiza, kwa mfano huko Ufaransa katika mtaguso wa Tours (567) na ule wa Mâcon (585).

Hatimaye Papa Adrian I alipitisha maagizo hayo mwaka 787.

Baadaye njia za kuwategemeza viongozi wa Kanisa zilitofautiana kadiri ya nchi na madhehebu.

Katika Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Zakat ni mojawapo ya Nguzo Tano za Kiislamu, ambayo inadai muumini atoe sehemu fulani ya mapato yake kwa maskini.

Tendo hilo muhimu la kutoa msaada linatazamwa na Waislamu kama njia ya kujipatia utakaso wa uroho na ubinafsi na ya kubarikiwa katika riziki zao.

Katika Usingasinga[hariri | hariri chanzo]

Katika dini ya Sikh muumini anadaiwa kutoa dasvand (ਦਸਵੰਦ) maana yake moja kwa kumi. Inaonekana sheria hiyo ilitokana na Uislamu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: