Nenda kwa yaliyomo

Wakfu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Genevieve akiwekwa wakfu na askofu: mchoro wa mwaka 1821 (Ste. Genevieve, Missouri).

Wakfu (kwa Kiarabu وقف‎‎) inamaanisha hali ya kutengwa na matumizi mengine, hasa kwa ajili ya matumizi ya kidini au manufaa kwa umma tu.

Watu, vitu na mahali wanaweza kuwekwa wakfu kwa namna mbalimbali.

Maana ya Kisheria[hariri | hariri chanzo]

Kwa maana ya kisheria wakfu (kwa Kiingereza foundation au charitable trust) ni taasisi au shirika lililopokea mali au pesa kwa matumizi ya manufaa kwa umma.

Sheria za Kenya[1] zinaruhusu mali kuwekwa wakfu kwa manufaa ya dini, elimu, utamaduni, sayansi, jamii, michezo au usaidizi wa watu maskini[2].

Mali ya taasisi ya aina hiyo imo mikononi mwa wadhamini (ing. trustees) wenye wajibu wa kutunza mali ya wakfu kwa madhumuni yaliyoelezwa katika hati ya taasisi na kuandikishwa katika ofisi ya serikali.

Kimsingi taasisi ya wakfu ilipokea mali ambayo ni msingi wa kazi yake, kwa mfano ardhi, majengo, hisa au pesa. Kuna pia mifano ya taasisi za wakfu zisizo na rasilmali zikitafuta zaidi michango ya wafadhili kwa ajili ya kazi yao kulingana na madhumuni. [3]

Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Katika Ukristo, watu wanaweza kuwekwa wakfu, hasa kwa njia ya sakramenti zisizoweza kurudiwa kwa sababu zinatia alama isiyofutika milele (yaani ubatizo, na kwa madhehebu mengine pia kipaimara na daraja takatifu), lakini pia kwa kushika maisha ya pekee katika useja mtakatifu (kwa kawaida pamoja na ufukara na utiifu).

Vitu na mahali vinaweza kuwekwa wakfu hasa kwa ajili ya ibada, k.mf. vyombo vya ibada, mavazi ya ibada na kanisa.

Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Katika Uislamu wakfu ni mali iliyotengwa kwa kusudi la kidini. Mifano ya wakfu ni kutoa kiwanja kwa kujenga msikiti, shamba au nyumba ikiwa mapato yake yatagharamia misikiti, madrasa, hospitali, watu maskini au wanafunzi, au pia kutoa pesa kwa makusudi haya.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Establishment of charitable foundation, fungu '(B) ADVICE ON INCORPORATION OF A FOUNDATION UNDER THE TRUSTEES (PERPETUAL SUCCESSION) ACT
  2. "for any religious, educational, literary, scientific, social, athletic or charitable purpose", ( (Trustees Act Cap. 164 Section 3(1), Kenyanlawyer.blogspot,angalia juu)
  3. Private Foundations and Development Cooperation, Insights from Tanzania, Erik Lundsgaarde na wengine, German Development Institute , Bonn 2012, ukurasa 48-49 hasa

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakfu kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.