Melkisedek

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkutano wa Abrahamu na Melchisedek kadiri ya Dieric Bouts Mzee, 14641467.

Melkisedek (kwa Kiebrania מַלְכִּי־צֶדֶֿק, Malkī-ṣeḏeq, yaani "Mfalme wangu ni haki") alikuwa mfalme wa Salemu, Kanaani, katika karne ya 19 KK.

Ni maarufu hasa kwa sababu sura ya 14 ya Kitabu cha Mwanzo katika Biblia ya Kiebrania inasimulia alivyompongeza na kumbariki Abrahamu aliporudi mshindi kutoka vitani.

Humo anatambulishwa pia kama kuhani wa El Elyon ("Mungu Aliye Juu") aliyemtolea sadaka ya mkate na divai.

Hatimaye Abrahamu alimgawia sehemu ya kumi ya mateka yake.

Habari hiyo ikawa hoja kwa wafalme wa Yerusalemu kuanzia Daudi ya kutetea mamlaka yao katika mambo ya ibada (Zab 110:4), ambayo Torati iliwaachia Walawi, hasa wa ukoo wa Haruni.

Hatimaye Waraka kwa Waebrania unazungumzia kirefu habari hizo ili kutetea ukuhani mkuu wa Yesu Kristo, Mwana wa Daudi.

Anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 26 Agosti[1][2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Melkisedek kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.