Nenda kwa yaliyomo

Mwana wa Daudi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Samueli akimpaka mafuta Daudi kati ya kaka zake: mchoro wa karne ya 3 huko Dura Europos, Syria.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Mwana wa Daudi ni jina la heshima la wanaume waliotokana na vizazi vya mfalme Daudi na hivyo kuhusishwa na ahadi alilopewa na nabii Nathani kwamba ukoo wake utatawala milele (2Sam 7:1-29).

Wengi wa nasaba hiyo waliotawala baada ya Daudi walishindwa vibaya katika jukumu lao la kufanya Waisraeli wazidi kuwa waaminifu kwa Mungu pekee, hivyo walisababisha kwanza farakano la kudumu katika taifa lao na hatimaye maangamizi yaliyoacha nchi takatifu bila wakazi waliotarajiwa na bila mtawala kutoka ukoo wa Daudi.

Ndiyo sababu manabii walizidi kuelekeza Wayahudi kutumaini uaminifu wa Mungu utakaotokeza mfalme bora kama chipukizi kutoka kisiki cha Yese, baba wa Daudi.

Hivyo, kwa namna ya pekee, jina hilo lilitumika kwa Yesu aliyetambuliwa na wengi, ama wakati wa maisha yake au baada ya kifo chake, kuwa ndiye Masiya aliyetazamiwa.

Injili ya Mathayo na Injili ya Luka zinasisitiza haki ya Yesu kuitwa hivyo kwa kuorodhesha vizazi kati ya Daudi na Yosefu, mume wa Bikira Maria, mama yake.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwana wa Daudi kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.