Vita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Vita: Mfalme Ramses II mnamo 1274 KK, Mfalme Gustav Adolf mnamo 1623, Faru ya Marekani M1 2005

Vita ni mapambano baina nchi, mataifa au angalu vikundi vikubwa vya watu yanayoendeshwa kwa nguvu ya silaha.

Mchoro wa Pier Gerlofs Donia na Wijerd Jelckama wakipigana kwa ajili ya uhuru wa watu.

Katika vita kuna pande mbili au zaidi. Husababisha mateso, vifo na kuharibika kwa mali ya watu pamoja na mazingira asilia.

Mwanamgambo wa Kipalestina akiwa ameshika silaha aina yaM16 rifle, mwaka 2009

Aina za vita[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina nyingi za vita:

 • vita kati ya nchi kwa niaba ya serikali zao
 • vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi
 • vita ya watu wa sehemu moja ndani ya nchi dhidi ya serikali
 • vita ya watu wa koloni au nchi lindwa dhidi ya serikali ya kikoloni au nchi inayotawala

Asili ya vita ilikuwa mapambano kwa silaha kati ya makabila au vijiji mbalimbali. Baada ya kutokea kwa madola ilikuwa zaidi serikali au watawala wa madola walioamua juu ya vita.

Mlipuko wa silaha ya nyuklia 1951

Watekelezaji wa vita[hariri | hariri chanzo]

Watekelezaji wa vita huitwa askari au wanajeshi. Historia imejua vipindi ambako wanaume wote wa nchi fulani walitakiwa kushika silaha na kushiriki katika mapigano. Palikuwa pia na vipindi na utamaduni ambako wapiganaji walikuwa watu wa pekee wenye jukumu hii ama kwa sababu walipaswa kuwa askari kufuatana na sheria za nchi au kwa sababu walikodiwa kwa kazi hii.

Wanajeshi rasmi huwa chini ya kanuni za vita lakini sehemu kubwa na vita inashirikisha watu wasofuata kanuni hizi kama wanamigambo hasa katika vita za wenyewe kwa wenyewe.

Silaha[hariri | hariri chanzo]

Wanadamu wametumia akili nyingi kuboresha vifaa vya vita yaani silaha na mbinu za vita. Maendeleo ya silaha yamesababisha kupungua kwa idadi ya askari wanaopigana moja kwa moja lakini uharibifu wa silaha umeongezeka.

Silaha za kale zilitegemea nguvu ya mkono wa mtu zikifikia umbali mdogo. Silaha zimebadilika kulenga mahali ambapo ni mbali na mbali zaidi. Silaha kali za kisasa zina uwezo wa kuharibu nchi yote; jumla ya silaha za nyuklia inatosha kuua maisha yote duniani.

Jitihada za kupakana vita[hariri | hariri chanzo]

Kutokana uharibifu mkubwa unaosababishwa na vita palikuwa tena na tena na makubaliano juu ya kanuni za vita. Kanuni hizi hulenga kupakana hasara inayosababishwa na mapigano. Lakini historia inajaa pia mifano ambako kanuni hizi zilivunjwa au kupuuzwa.

Katika karne ya 20 mataifa mengi yalipatana mikataba ya kimataifa juu ya kanuni za vita. Chanzo ilikuwa Mapatano ya Geneva baada ya kuundwa kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu mwaka 1863.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia nchi nyingi ziliunda Shirikisho la Mataifa kwa shabaha ya kuzuia vita lakini hii ilishindikana baada ya nchi kubwa kama Urusi, Ujerumani na Italia kupuuza maazimio yake. Kuundwa kwa Umoja wa Mataifa kulikuwa jaribio jipya la kuwa na taasisi ya kimataifa yenye uwezo wa kuzuia vita.

Vasili Vereshchagin: Ufaulu wa Vita (1871)

Misemo juu ya vita[hariri | hariri chanzo]

 • "Inawezekana kuanza vita unapotaka lakini haiwezekani kuimaliza unapotaka." - Niccolò Machiavelli
 • "Vita ni baba wa vitu vyote." - Heraklitos
 • "Vita ni aina ya siasa kwa kutumia mbinu tofauti." - Carl von Clausewitz
 • "Ukitaka amani andaa vita." - Vegetius
 • "Si vita bali amani ni baba wa vitu vyote." - Willy Brandt
 • "Vita abadan!" - Yohane Paulo II
 • "Vita ilipokwisha askari alirudi nyumbani. Lakini alipokosa chakula akamwona mwenye chakula. Akamwua. "Lakini huruhusiwi kumwua mtu!" alisema hakimu. "Kwa nini?" aliuliza askari." - Wolfgang Borchert