Vasili Vereshchagin
Vasili Vasilyevich Vereshchagin (Kirusi: Василий Василиевич Верещагин; 26 Oktoba 1842 - 13 Aprili 1904) alikuwa mchoraji kutoka Urusi aliyefahamika sana kutokana picha zake za vita na mapigano.
Alikuwa mtoto wa mkulima aliyepata elimu kwenye shule ya kijeshi akandelea kuwa afisa wa jeshi la Urusi. Aliondoka jeshini akawa mwanafunzi wa uchoraji huko Sankt Peterburg akamaliza masomo yake kwenye Chuo cha Sanaa mjini Paris.
Kama afisa wa jeshi alipata nafasi ya kuongozana na jeshi la Kirusi kwenye kempeni zake katika Asia ya Kati. Aliona vita kali na mauaji mengi akaamua kuonyesha uharibifu wa vita kwa umakini kwa matumaini ya kwamba watu wangekataa vita baada ya kuona ubaya wake. Kwa hiyo alichora mara nyingi maiti, askari wajeruhiwa, uharibifu wa vijiji na mahospitali.
Sehemu ya picha zake zilifichwa baadaye na serikali ya Kirusi.
Alifariki wakati wa vita ya Japani dhidi ya Urusi ya 1904-1905 aliposafiri kwa manowari ya Kirusi iliyozamishwa na Wajapani. Picha yake ya mwisho aliyochora kwenye manowari iliokolewa kutoka katika maji.
-
Madervish wakivaa mavazi ya sikukuu (1870)
-
Shambulio la ghafla,
Picha kutoka Turkestan (1871) -
Kuhusu vita,
Picha kutoka Turkestan (1873) -
Napoleon kwenye mapigano ya Borodino (1897)
-
Uzuri wa vita (1871)
-
Uwanja wa mapigano
-
Mauaji wa Masepoy (1857)
-
Washindi (1878-1879)