Italia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Repubblica Italiana
Jamhuri ya Italia
Bendera ya Italia Nembo ya Italia
Lugha rasmi Kiitalia; kijimbo pia Kijerumani, Kifaransa, Kiladino, Kislovenia, Kisardinia
Mji Mkuu Roma
Rais Sergio Mattarella
Waziri Mkuu Matteo Renzi
Eneo 301.338 km²
Wakazi 60,782,668 (31-7-2013) (23º duniani)
Wakazi kwa km² 201.7
JPT 31,022 US-$ (2008)
Pesa Euro
Wakati UTC+1
Wimbo wa Taifa Fratelli d'Italia (Ndugu wa Italia)
Sikukuu ya Jamhuri 2 Juni
Sikukuu ya Taifa 25 Aprili
Simu ya kimataifa +39
Italia katika Ulaya na katikati ya Bahari ya Kati.
Ramani ya Italia
Italia jinsi inavyoonekana kutoka angani

Jamhuri ya Italia ni nchi ya Ulaya Kusini. Eneo lake ni 301.338 km² ambalo lina wakazi 60,782,668 (31-7-2013): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 12 kwa uchumi.

Makao makuu ni jiji la Roma, lenye umuhimu mkubwa katika historia ya dunia nzima.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Umbo lake linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu.

Visiwa viwili vikubwa vya Sicilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vidogovidogo.

Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia.

Nchi huru mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia pande zote ni San Marino na Vatikano.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 K.K.), lakini hiyo ilipoenea Ulaya, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa.

Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa Roma (476) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu.

Juhudi za kuurudisha zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870).

Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.

Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa la pamoja (Euro).

Maendeleo[hariri | hariri chanzo]

Italia ni nchi iliyoendelea, ikiwa na nafasi ya nane kwa nguvu ya kiuchumi duniani, hivyo ni mwanachama wa G7, G8 na G20.

Sanaa na utalii[hariri | hariri chanzo]

Pia ni nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (45) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".

Kwa sababu hiyo pia inashika nafasi ya 5 kati ya nchi zote zilizo lengo la utalii.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wananchi wana sifa za pekee kati ya Wazungu wote, hata upande wa DNA, kutokana na historia ya rasi.

Lugha rasmi ni Kiitalia, inayotegemea zaidi lahaja za Italia ya Kati, lakini siku hizi inatumiwa na wananchi walio wengi hata katika mikoa mingine, ambayo kwa jumla ni 20.

Wengi wao (81.2%) ni Wakristo wa Kanisa Katoliki, wakifuatwa na Waorthodoksi (2.5%, wengi wao wakiwa wahamiaji hasa kutoka Romania). Uhamiaji mwingi wa miaka ya mwisho wa karne ya 20 umeleta pia Uislamu (2.6%) na dini nyingine.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vyo nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Italy looking like the flag.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.