Ibada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sehemu ya mchoro Dini wa Charles Sprague Pearce (1896).

Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalotolewa kwa Mungu au miungu.

Inaweza kufanywa na mtu binafsi au na kundi, hasa likiongozwa na kuhani au mwingine aliyekubalika.

Dini zinaelekeza binadamu kufanya ibada inavyotakiwa.

Ibada inasisitiza ukweli wa yule anayetolewa heshima hiyo, kwa mfano kutokana na imani ya dini fulani.[1]Vilevile ukweli wa mtoaji kwa maana ibada lazima itoke moyoni: ndiyo sababu haiwezi kulazimishwa.

Neno la Kiswahili linatokana moja kwa moja na Kiarabu ambapo neno عبادة, ibadah, linahusiana na maneno mengine kama vile "utumwa", na linadokeza utiifu na unyenyekevu hasa kwa Mungu pekee, inavyodaiwa na Uyahudi, Ukristo na Uislamu.[2]

Ukristo unasisitiza uhumimu wa kumuabudu Mungu kama Baba kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na kufuata ukweli uliofundishwa na Yesu Kristo.

Uislamu unaona ibada kuwa lengo lenyewe la uumbaji wa binadamu na majini.[3] Katika karne ya 13 mwanachuo Ibn Taymiyyah aliieleza ibada ni "neno pana linalojumlisha kila jambo ambalo Allah analipenda na anapendezwa nalo - lile usemi au matendo, ya nje na ya ndani".[4]

Wataalamu wa sosholojia wanaonyesha kwamba wasio na dini wanaweza wakaabudu mambo mengine kama vile timu ya mpira, chama cha siasa, taifa au wasanii mbalimbali.[5][6]

Katika Kiswahili neno linaweza kuwa na maana ya mazoea: "Kwake ulevi ni ibada".

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Nagata, Judith (Jun 2001). "Beyond Theology: Toward an Anthropology of "Fundamentalism"". American Anthropologist 103 (2).
  2. al-Qamoos al-Muhit
  3. Al-Qur'an 51:56.
  4. Majmu' al-Fatawa (10/149)
  5. http://sydney.edu.au/news/84.html?newsstoryid=10384
  6. http://www.cf.ac.uk/socsi/undergraduate/introsoc/durkheim6.html
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ibada kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.