Alpi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Alpi kutoka angani.

Alpi (Kijerumani: Alpen; Kifaransa: Alpes; Kiitalia: Alpi; Kislovenia: Alpe) ni safu ya milima katika Ulaya inayotenganisha Ulaya ya Kati na Ulaya ya Kusini.

Alpi zinaanza upande wa mashariki katika Austria na Slovenia, zikipita Italia ya kaskazini, Uswisi, Liechtenstein na Ujerumani hadi Ufaransa upande wa magharibi. Katika Austria a Uswisi Alpi zafunika sehemu kubwa ya eneo la nchi.

Mlima wa juu ni Mont Blanc ("mlima mweupe") mpakani wa Ufaransa na Uswisi mwenye kimo cha mita 4,808 juu ya UB.

Alpi ni safu yenye umri mdogo kijiolojia wa miaka milioni 30-35. Safu ilijikunja na kupaaa juu kwa sababu bamba la Afrika inagongana na bamba la Ulaya na Alpi zaendelea kujikunja na kukua milimita 1-2 kila mwaka.

Vilele vya juu vina theluji na barafu za kudumu yaani mwaka wote. Isipokuwa ukubnwa wa barafuto za Alpi hupungua haraka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Alpi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.