Kiitalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kiitalia ni lugha inayozungumzwa na watu milioni 70 hasa nchini Italia.

Ni lugha rasmi ya Italia, San Marino, Vatikano, Uswisi na katika sehemu za Slovenia na Kroatia.

Inatumika pia katika Monako, Malta, Albania na visiwa kadhaa za Ugiriki), halafu bado kama lugha ya elimu katika nchi zilizokuwa koloni za Italia kama Eritrea, Libya, Ethiopia na Somalia.

Kihistoria asili yake ni lugha ya Kilatini. Pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania na lugha ndogo ni moja ya lugha za Kirumi.

Blau: Amtssprache; Hellblau: Verkehrssprache ItalophoneEuropeMap.png
Kiitalia