Bamba la Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bamba la Afrika (nyekundu-njano) kati ya mabamba gandunia ya dunia yetu
Ramani ya Afrika ya Mashariki inayoonyesha volkeno kadhaa (pembetatu nyekundu) na pembetatu ya Afar - eneo la kuachana kwa bamba la Uarabuni na bamba la Afrika linalojipasua hapa kuwa bamba la Afrika ya Kinubia na la Afrika ya kisomalia.

Bamba la Afrika ni kati ya mabamba makubwa ya gandunia ya dunia yetu. Lipo chini ya bara la Afrika na chini ya sehemu za bahari zinazopakana nalo yaani tako la bara.

Bamba hili limepakana na bamba la Ulaya-Asia, bamba la Uarabuni, bamba la Uhindi, bamba la Australia, bamba la Antaktika na bamba la Amerika ya Kaskazini. Inawezekana ya kwamba limepakana na mabamba madogo mengine yasiyoeleweka bado.

Bamba la Afrika lina mwendo wa kuelekea kaskazini unaopimwa kuwa 2.15 cm kila mwaka. Kwa mkasi huu bara la Afrika litagusana na Hispania ya Kusini baada ya miaka 650,000 na kufunga mlango wa bahari ya Gibraltar hivyo kufunga Mediteranea na kuifanya kuwa ziwa.

Bamba la Afrika yenyewe liko katika mwendo wa kupasuliwa kwenye mstari wa ufa la Afrika ya Mashariki kutoka Eritrea kupitia Ethiopia, Kenya, Tanzania, Malawi na mwishowe katika Msumbiji. Sehemu mbili za bamba la Afrika huitwa na wataalamu bamba la Afrika ya Kinubia na la Afrika ya kisomalia.

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Bamba la Afrika" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.