Bahari ya Mediteranea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mediteranea)
Bahari ya Mediteranea jinsi inavyoonekana kutoka chombo cha angani
Ramani ya Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Bahari ya Mediteranea ni bahari, si ziwa, kwa sababu imeunganishwa na Atlantiki kwa njia ya mlango wa bahari wa Gibraltar.

Ina bahari za pembeni zake ambazo ni pamoja na Bahari Nyeusi, Bahari ya Aegean, Bahari ya Tyrrheni na mengine. Bahari Nyeusi inaunganishwa kwa njia ya mlangobahari wa Dardaneli, Bahari ya Marmara na mlangobahari wa Bosporus.

Tangu mwaka 1869 kuna pia njia ya maji kati ya Mediteranea na Bahari ya Shamu ambayo ni Mfereji wa Suez.

Kuna visiwa vingi sana hasa kati ya Ugiriki na Uturuki. Visiwa vikubwa ni Korsika, Sardinia, Sisilia, Kreta, Rhodos na Kibros.

Nchi zinazopakana[hariri | hariri chanzo]

Leo hii kuna nchi au madola 22 zinazopakana na Bahari ya Mediteraneo:

Misri, Libya, Tunisia, Algeria na Moroko
Uturuki, Syria, Lebanon, Israel, Kibros (Cyprus, kisiwa), Palestina (Gaza) na Misri
Hispania, Ufaransa, Monako, Italia, Malta (funguvisiwa), Slovenia, Kroatia, Bosnia - Herzegovina, Montenegro, Albania, Ugiriki, Uturuki

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons