Eritrea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
ሃግሬ ኤርትራ
Hagärä Ertra
Flag of Eritrea
(Kinaganaga) (Kinaganaga)
Hadabu ya Taifa: Nie nie
Location of Eritrea
Lugha za Taifa Tigrinya, Kiarabu
na Kiingereza
Mji Mkuu Asmara
Rais Isaias Afwerki
Eneo
 - Total
 - % Maji
Kadiriwa 101th
117,600 km²
Acha
Idadi ya Watu
 - Makadirio (2014)
 - Jumla (2002)
 - Chumo cha Umma kugawa na Eneo
Kadiriwa 107th
6,380,803
4,298,269
51.8/km² (154th)
GDP (PPP)
 - Jumla
 - Kwa Kila Raia (Per capita)
2005 estimate
4,250 (155th)
917 (177th)
Uhuru
 - Kadirifu
 - Barabara
Kutoka Ethiopia (Uhebeshi)
 Mai 29, 1991
 Mai 24, 1993
Fedha Nakfa
Saa za Eneo UTC +3
Wimbo wa Taifa Ertra, Ertra, Ertra
Intaneti TLD .er
Kodi ya simu 291

Eritrea ni nchi ya Afrika kaskazini-mashariki.

Upande wa Magharibi imepakana na Sudan, upande wa Kusini imepakana na Ethiopia, na Kusini-Mashariki kuna nchi ya Djibouti. Mashariki na Kusini-Mashariki Eritrea ina pwani ndefu ya Bahari ya Shamu. Eneo hili lote hujulikana pia kama Pembe ya Afrika.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la nchi limetungwa mnamo mwaka 1890 na wakoloni wa Italia kutokana na neno la Kigiriki "erythraîa" linalomaanisha “bahari nyekundu”. Hii ni kwa sababu Bahari ya Shamu iliitwa "Sinus Erythraeus" na mabaharia Wagiriki au “Mare Erythraeum” kwa Kilatini na Waroma wa kale – maana yake ni "bahari nyekundu" – tazama Kiingereza “Red Sea”.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Angalia makala: Historia ya Eritrea

Historia ya Eritrea kama eneo la pekee, jinsi lilivyopata uhuru mwisho wa karne ya 20, ilianza na ukoloni wa Italia.

Hadi karne ya 19 maeneo ya Eritrea yalikuwa sehemu ya Ethiopia.

Pwani ilikaa karne nyingi chini ya utawala wa Uturuki au baadaye Misri zilizokuwa nchi zenye nguvu kwenye Bahari ya Shamu.

Koloni la Italia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1869 kampuni la Kiitalia lilinunua bandari ya Assab ambayo ikawa koloni la serikali ya Italia mwaka 1882.

Italia ilipanua utawala wake kwa kutwaa mji wa Massawa mwaka 1885 na kuchukua pia pwani yote kati ya miji hiyo miwili.

Baadaye Waitalia walianza kuelekea nyanda za juu na Ethiopia yote.

Mwendo huo ulisimamishwa na Ethiopia katika mapigano ya Adowa mwaka 1896. Italia ilikubali uhuru wa Ethiopia, nayo ilikubali koloni la Italia katika Eritrea.

Koloni lilianzishwa rasmi mwaka 1890 kwa jina la "Eritrea" kutokana na jina la kale la "Mare Erytraeum" au Bahari ya Eritrea.

Utawala wa Italia ulileta mabadiliko mengi kati ya watu wa koloni na kujenga jamii mpya na tofauti na wakazi wa Ethiopia, hivyo kuweka msingi wa taifa la pekee.

Tangu mwaka 1922 serikali mpya ya Italia ya Mussolini ilianzisha siasa ya ubaguzi wa rangi na kuwatendea wenyeji kwa dharau.

Kuanzia mwaka 1935 Eritrea ilikuwa mahali pa kuanzisha vita vipya vya Italia dhidi ya Ethiopia.

Eneo lindwa la Uingereza[hariri | hariri chanzo]

Katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia jeshi la Italia katika Ethiopia lilishindwa na Waingereza na Eritrea ikaja kutawaliwa na Uingereza tangu 1941 mpaka 1952, Eritrea ilipokabidhiwa na Umoja wa Mataifa kwa Ethiopia kama eneo la pekee.

Chini ya Ethiopia[hariri | hariri chanzo]

Serikali ya Haile Selassie ililenga kuunganisha tena Eritrea na Ethiopia na kwa mbinu mbalimbali ilipata kura ya bunge la Eritrea ya kujivunja na kuwa jimbo la Ethiopia.

Baada ya tukio hilo vikundi vya wanamgambo walienda porini kupigania uhuru wa Eritrea kwa silaha.

Baada ya vita vya miaka 30 harakati ya Eritrean People's Liberation Front (EPLF) ilishinda jeshi la Ethiopia mwaka 1991. Ushindi huo ulikuwa baadaye sababu kuu ya kuanguka kwa serikali ya Ukomunisti ya Ethiopia.

Eritrea huru[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kura ya wakazi wa Eritrea, uhuru wa nchi ilitangazwa tarehe 24 Mei 1993. Awali uhusiano na serikali mpya ya Ethiopia ulikuwa mzuri, lakini baada ya miaka ya kwanza ulizorota.

Mwaka 1998 kulitokea vita kati ya Eritrea na Ethiopia vilivyokwisha na ushindi wa Ethiopia. Wanajeshi wa kulinda amani wa UM wanajaribu kutunza hali ya kutopigana.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Kifungu chenyewe: Siasa za Eritrea
Rais wa Eritrea, Isaias Afewerki (kulia) na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Donald Rumsfeld.

Bunge la Taifa la viti 150, liliyotekezwa mwaka 1993 baada ya Uhuru, lilimchagua Rais wa sasa, Isaias Afewerki. Kura za Nchi huwa zinapangwa na kupanguliwa.

Shina za taarifa madaraka za kutangaza habari kwa siasa za nyumbani Eritrea haziko; na Septemba 2001 serikali ilifunga vyombo vya habari midia vya binafsi, na watu wanaopinga serikali kufungwa bila kushtakiwa, hii yote ni kutoka taarifa ya washufu wa ulimwengu, kama Waangalizi wa haki za Kibinadamu (Human Rights Watch) na Wakombozi wa Kimataifa (Amnesty International).

Mambo ya nje yanahusu vita na Ethiopia na Sudan. Baada ya wajumbe wa serikali ya Eritrea wa Idara ya mambo za kigeni kuenda Sudani, ushirikiano umeanza kuwa wa kawaida. Bishano na Ethiopia bado ni mawazo makubwa ya chuki ambayo imemfanya Rais kuuambia Umoja wa Mataifa ichukuE hatua. Uagizaji huu umeElezwa kwa barua kumi na moja uaNdishi wa Rais[1].

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Kifungu chenyewe: Maeneo ya Eritrea

Eritrea imegawiwa katika maeneo 6:

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eritrea
Kifungu chenyewe: Jiografia ya Eritrea

Eritrea iko katika eneo la Pembe la Afrika na imepakana na Bahari ya Shamu kaskazini mashariki. Kwa mchanga wa pwani uliyo Eneo Kame pahali pa kutega samaki ni Dahlak Achipelago.

Eneo ambalo liko kwa milima kusini si kame vile, lakini hali ya hewa ni poa. Mlima wa juu zaidi ni Soira, ambao uko kati ya Nchi Eritrea, mita 3018 juu ya bahari.

Mji mkuu wa Eritrea ni Asmara na miji mingine ni kama vile mji wa bandari Assab kusini mashariki, na pia miji kama Massawa na Keren.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa Eritrea walikadiriwa kuwa 6,380,803 mwaka 2014.

Makabila makubwa ni Watigrinya (55%) na Watigre (30%), ambao wote wawanazungumza lugha za Kiafrika-Kiasia.

Nchi haina lugha rasmi ili kuheshimu sawasawa lugha zote. Hata hivyo Kitigrinya, Kiarabu na Kiingereza vina nafasi za pekee.

Serikali inatambua rasmi Kanisa la Kiorthodoksi la Eritrea, Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri pamoja na Uislamu. Makadirio yanatofautiana: Wakristo kwa jumla ni 50-68%, Waislamu 36-48%.

Mwaka 2004 Idara ya taifa ya Marekani (U.S. State Department) iliamua kwamba Eritrea ni Nchi mahsusi ya kufuatiliwa (Country of Particular Concern, au CPC) kwa kufinya uhuru wa dini.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eritrea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.