Malawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Dziko la Malaŵi (Chichewa)
Republic of Malawi (engl.)
Jamhuri ya Malawi
Bendera ya Malawi
Bendera ya Malawi
Coat of arms of Malawi.svg
Lugha rasmi Chichewa, Kiingereza
Mji Mkuu Lilongwe
Serikali Jamhuri
Rais Peter Mutharika
Eneo 118.480 km²
Wakazi 12.158.924 (Julai 2005)
Wakazi kwa km² 102
JPT/Mkazi 157 US-$ (2004)
Uhuru kutoka Uingereza tar. 06.07.1964
Pesa Kwacha ya Malawi
Wimbo wa Taifa Mlungu salitsani Malawi
Malawi katika Afrika
Ramani ya Malawi

Makala hii inahusu nchi ya Malawi. Kwa maana mbalimbali za neno taz. Malawi (maana)


Malawi (zamani Unyasa au Nyasaland) ni nchi ya Afrika ya kusini-mashariki ikipakana na Tanzania, Msumbiji na Zambia. Jina la nchi limeteuliwa kutokana na ufalme wa Maravi. Wakati wa ukoloni iliitwa Unyasa. Sehemu kubwa ya eneo lake ni ziwa kubwa linaloitwa "Ziwa Nyasa" au "Niassa" na majirani lakini "Ziwa Malawi" hapa nchini. Kuna mzozo kati ya Malawi na Tanzania kuhusu eneo la ziwa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza wa Malawi walikuwa wavindaji Wasan. Katika karne za kwanza BK wahamiaji Wabantu walifika wenye ujuzi wa kilimo na uhinzi.

Hakuna habari za kimaandishi kabla ya kufika kwa Wazungu. Tangu karne ya 16 BK ufalme wa Wamaravi ulikuwepo upande wa kusini wa ziwa. Wamaravi walipanusha utawala wao. Lakini katika karne ya 19 BK walishambuliwa sana na Wayao walioendesha biashara ya watumwa wakiwakamata katika eneo la ziwa na kuwapeleka pwani la Bahari Hindi kama Kilwa.

Mwaka 1859 Mwingereza David Livingstone alifika ziwani. Wamisionari walimfuata hasa Wapresbiteri kutoka Uskoti waliotafuta wafuasi wa Ukristo na kumpambana na wafanyabiashara na umtumwa. Mwaka 1891 serikali ya Uingereza iliweka nchi upande wa magharibi na kusini ya ziwa chini ya ulinzi wake ikawa „Nyassaland Protectorate“, tangu 1907 koloni ya Unyasa. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waingereza waliogopa kushambuliwa kutoka Afrika ya Mashariki ya Kijerumani wakachukua hatua za kudai huduma za nyongeza kutoka kwa wanachi. Hii ilisababisha ghasia ya John Chilembwe dhidi ya wakoloni.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza waliunganisha Unyasa na Rhodesia (Zambia na Zimbabwe) kuwa Shirikisho la Afrika ya Kati mwaka 1953. Shirikisho hili halikudumu hadu mwisho wa ukoloni kutokana mielekeo tofautitofauti katika sehemu zote tatu za shirikisho.

Katika Unyasa daktari Hastings Kamuzu Banda alijitokeza kuwa mwanasiasa aliyependelewa na wananchi wengi akawa waziri mkuu wakati wa Unyasa kupata madaraka ya kujitawala katika mambo ya ndani na baadaye rais wa kwanza wa Taifa. 1964 Unyasa (Nyassaland) ilkuwa nchi huru kabisa lakini bado sehemu ya Jumuiya ya Madola chini ya malkia wa Uingereza. 1966 Banda alitangaza kura ya katiba mpya iliyopokelewa nach wananchi. Nchi imepata jina la Malawi na chama cha Malawi Congress Party kikawa chama cha pekee.

Banda aliendelea kutawala akatangazwa kuwa rais kwa muda wa maisha yake mw. 1971. Mabadiliko ya kimataifa baada ya kuporomoka kwa Ukomunisti na ukuta wa Berlin 1989/1990 yalileta shindikizo kote Afrika dhidi ya serikali zilizofuata mtindo wa chama kimoja- Shindikizo hili lilimkuta Banda mzee na mgonjwa ilhali watu wa familia yake wakitawala kupitia yeye. Hali ya uchumi ilikuwa duni, rushwa na magendo juu.

Mwaka 1993 serikali yake ililazimishwa kukubali kura ya wanachi wote walioamua kumaliza mfumo wa chama kimoja na kuanzisha kipindi kipya. Uchaguzi huru wa 1994 ulimaliza utawala wa MCP ukamfanya Bakili Muluzi wa United Democratic Front (UDF) ndiye rais aliyechaguliwa mara ya pili 1999 . Katika uchaguzi wa 2004 alishinda tena mgombea wa UDF ndiye Bingu Mutharika aliyeapishwa kuwa rais wa Malawi tar. 24. Mei 2004 huko Blantyre

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Malawi ilikuwa na siasa ya chama kimoja chini ya rais wa kwanza Hastings Kamuzu Banda tangu kupata uhuru mwaka 1964 na masahihisho ya katiba 1966.

Tangu kura ya wananchi mwaka 1993 Malawi imeanzisha mfumo wa vyama vingi vya kisiasa. Kutokana na katiba ya 1995 rais wa taifa anayechaguliwa na wananchi ndiye mkuu wa dola pia mkuu wa serikali. Makamu wa rais anachaguliwa pamoja naye lakini rais ana haki ya kumteua makamu wa pili asiyetoka katika chama chake.

Mawaziri huteuliwa ama kati ya wabunge au nje ya bunge.

Wabunge 193 wanachaguliwa moja kwa moja na wanachi kwamuda wa miaka mitano.

Mahakama zinafuata mtindo wa Uingereza. Majaji huteuliwa kwa muda wa maisha wanatakiwa kuwa huru na kutoathiriwa na siasa.

Utawala hutekelezwa katika mikoa mitatu ya nchi zinazogawiwa katika wilaya 28. Wakuu wa mikoa na wilaya huteuliwa na serikali kuu. Novemba 2000 palitokea uchaguzi wa kwanza wa ngazi ya chini mjini na vijijini.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Malawi ina mikoa mitatu ya Kaskazini, Kati na Kusini. Kuna wilaya 27. Chini ya ngazi ya wilaya kuna tarafa na vijiji vinavyoitwa maeneo ya machifu madogo.

Wilaya ndizo: Balaka Blantyre Chikwawa Chiradzulu Chitipa Dedza Dowa Karonga Kasungu Likoma Lilongwe Machinga Mangochi Mchinji Mulanje Mwanza Mzimba Nkhata Bay Nkhotakota Nsanje Ntcheu Ntchisi Phalombe Rumphi Salima Thyolo Zomba

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malawi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.