Burkina Faso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Burkina Faso
Bendera ya Burkina Faso Nembo ya Burkina Faso
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unité, Progrès, Justice (kwa Kifaransa: Umoja, Maendeleo, Haki)
Wimbo wa taifa: Une Seule Nuit (Usiku mmoja tu)
Lokeshen ya Burkina Faso
Mji mkuu Ouagadougou (Wagadugu)
13°00′ N 2°00′ W
Mji mkubwa nchini Ouagadougou
Lugha rasmi Kifaransa
Serikali Jamhuri
Paul-Henri Sandaogo Damiba
Albert Ouédraogo
Uhuru
 - Tarehe
Kutoka Ufaransa
5 Agosti 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
274,200 km² (ya 74)
0.146%
Idadi ya watu
 - 2020 kadirio
 - 2006 sensa
 - Msongamano wa watu
 
20,835,401 (ya 61)
14,017,2620
64/km² (145)
Fedha Franki ya CFA (XOF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC)
(hawafuati) (UTC)
Intaneti TLD .bf
Kodi ya simu +226

-

1 Namba hizi ni kadirio ya IMF kwa mwaka 2005.


Ramani ya Burkina Faso.
Ramani ambayo inaonyesha mikono ya mto Volta nchini.

Burkina Faso ni nchi ya Afrika ya Magharibi isiyo na pwani kwenye bahari yoyote.

Imepakana na nchi zifuatazo: Mali upande wa kaskazini, Niger upande wa mashariki, Benin, Togo, Ghana na Côte d'Ivoire upande wa kusini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya awali[hariri | hariri chanzo]

Koloni la Wafaransa[hariri | hariri chanzo]

Nchi ilianzishwa na Wafaransa kwa njia ya kugawa koloni la Cote d'Ivoire mwaka 1919. Jina la koloni jipya lilikuwa Volta ya Juu (kwa Kifaransa: Haute Volta). Jina limetokana na mto Volta unaoanzia hapa.

Kati ya miaka 1932 na 1947 eneo lake lilitawaliwa na makoloni ya jirani.

Baada ya uhuru[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1960 nchi ikawa huru.

Kiongozi wa nchi Thomas Sankara alibadilisha jina la nchi tarehe 4 Agosti 1984 kuwa Burkina Faso, yaani nchi ya watu waadilifu (kwa lugha ya Kimossi).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Eneo la Burkina Faso liko kwa kimo cha wastani ya mita 400 juu ya UB. Hakuna tofauti kubwa sana.

Mlima wa juu ni Ténakourou (katika kusini) wenye m. 749. Sehemu ya chini ni bonde la mto Pendjari mpakani kwa Benin.

Nchi iko kusini kwa pinde la mto Niger

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia: Orodha ya Miji ya Burkina Faso

Nchi imegawiwa kwa mikoa 13 (inaitwa region). Ndani ya mikoa kuna wilaya 45 (provinces) na tarafa 301 (departement). Kila mkoa husimamiwa na mkuu anayeitwa gouverneur.

Mito na maziwa[hariri | hariri chanzo]

Burkina Faso ina chanzo cha matawimto ya mto Volta ambayo ni Mouhoun (pia Volta Nyeusi), Nakambé (pia Volta Nyeupe) na Nazinon (pia Volta Nyekundu). Mouhoun ni mto pekee wenye maji mwaka mzima.

Sehemu za kaskazini na mashariki za nchi ambazo ni takriban robo ya eneo lake lote ni beseni yala mto Niger. Matawimto ya Niger (Béli, Gorouol, Goudébo na Dargol) yana maji kwa muda wa miezi 4-6 kila mwaka.

Kuna pia maziwa kadhaa, hasa Tingrela, Bam na Dem.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa ni ya kitropiki. Majira ya mvua ni kati ya Mei na Septemba.

Wakati wa kiangazi kuna upepo wa Harmattan unaotoka katika jangwa la Sahara.

Kuna kanda tatu ya hali ya hewa, kuanzia Sahel katika kaskazini hadi Sudan-Guinea katika kusini kwenye mvua zaidi.

Katika maeneo yabisi ya kaskazini serikali mbalimbali zimejitahidi kupanda miti, jumla ya milioni 23 katika miaka 1996-2000.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakulima wa Burkina Faso

Wakazi wa nchi huitwa "Waburkina" kutokana na jina la Burkina.

Idadi kubwa sana ya wananchi hukaa mashambani. Lakini miji inakua haraka.

Mji mkuu, Wagadugu, umeshapita idadi ya wakazi milioni moja.

Miji mingine muhimu ni Bobo-Dioulasso (wakazi 366,383), Koudougou (wakazi 89,374), Ouahigouya (wakazi 62,325) na Banfora (wakazi 61,762). (takwimu za Januari 2006)

Kabila kubwa nchini ni la Wamossi (karibu nusu ya wananchi wote) wakikaa karibu na Wagadugu. La pili ni la Wabobo hasa katika eneo la Bobo-Dioulasso. Kanda la Sahel katika kaskazini wako Wafula.

Lugha ya Kifaransa ndiyo lugha rasmi. Lugha kuu za mawasiliano ni Kimossi na Kidiula. Kwa ujumla kuna lugha 68 nchini Burkina.

Upande wa dini, wakazi Waislamu ni 63.8%, Wakristo ni 26.3% (Wakatoliki 20.1% na Waprotestanti 6.2%) na wafuasi wa dini asilia za Kiafrika ni 9%.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Engberg-Perderson, Lars, Endangering Development: Politics, Projects, and Environment in Burkina Faso (Praeger Publishers, 2003).
  • Englebert, Pierre, Burkina Faso: Unsteady Statehood in West Africa (Perseus, 1999).
  • Howorth, Chris, Rebuilding the Local Landscape: Environmental Management in Burkina Faso (Ashgate, 1999).
  • McFarland, Daniel Miles and Rupley, Lawrence A, Historical Dictionary of Burkina Faso (Scarecrow Press, 1998).
  • Manson, Katrina and Knight, James, Burkina Faso (Bradt Travel Guides, 2011).
  • Roy, Christopher D and Wheelock, Thomas G B, Land of the Flying Masks: Art and Culture in Burkina Faso: The Thomas G.B. Wheelock Collection (Prestel Publishing, 2007).
  • Sankara, Thomas, Thomas Sankara Speaks: The Burkina Faso Revolution 1983–1987 (Pathfinder Press, 2007).
  • Sankara, Thomas, We are the Heirs of the World's Revolutions: Speeches from the Burkina Faso Revolution 1983–1987 (Pathfinder Press, 2007).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Trade


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Burkina Faso kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.