Angola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República de Angola
Jamhuri ya Angola
Bendera ya Angola Nembo ya Angola
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Virtus Unita Fortior, kumaanisha "Kuunganisha maadili kunaongeza nguvu"
Wimbo wa taifa: Angola Avante!
(Kireno: Angola songa mbele!)
Lokeshen ya Angola
Mji mkuu Luanda
8°50′ S 13°20′ E
Mji mkubwa nchini Luanda
Lugha rasmi Kireno
Serikali Vyama vingi demokrasia
José Eduardo dos Santos
Paulo Kassoma
Uhuru
Kutoka Ureno
11 Novemba 1975
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,246,700 km² (23nd)
-
Idadi ya watu
 - [[]] kadirio
 - 1914 sensa
 - Msongamano wa watu
 
(71st)
24,383,301
14.8/km² (199)
Fedha Kwanza (AOA)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
- (UTC+1)
Intaneti TLD .ao
Kodi ya simu +244

-


Ramani ya Angola
Luanda, mji mkuu wa Angola

Angola ni nchi kubwa iliyopo upande wa kusini wa bara la Afrika ikipakana na Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Zambia. Upande wa magharibi kuna pwani ndefu ya Bahari Atlantiki. Mkoa wa Kabinda umetenganika na sehemu nyingine za nchi na unapakana na Jamhuri ya Kongo pia.

Angola ni nchi tajiri kwa mafuta na madini: almasi ndiyo muhimu zaidi. Lakini nchi ni maskini kutokana na vita vya miaka 29; kwanza vita vya kupigania uhuru dhidi ya Ureno iliyofuatwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 2002.

Nchi yenyewe hasa ni ya kidemokrasia na yajulikana kama Jamhuri ya Angola (Kireno: República de Angola, kwa kutamka IPA: /ʁɛ.'pu.βli.kɐ dɨ ɐ̃.'ɣɔ.lɐ/).

Asili na historia ya jina 'Angola'[hariri | hariri chanzo]

Jina Angola linatokana na lugha ya Kibantu neno N’gola, ambayo ilikuwa jina la kiongozi wa ufalme wa Kwimbundo karne ya 16, ambapo Wareno walianza ukoloni katika eneo hili.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia karne ya 16, falme mbalimbali zilienea sehemu za Angola, kwa mfano Dola la Lunda na Dola la Kasanje.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Kaulimbiu ya Angola ni "Virtus, Unita Fortior", kumaanisha "umoja utupe nguvu"

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Maeneo ya Angola[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Angola na Mikoa iliohesabiwa
Makala kuu: Mikoa ya Angola
,
Makala kuu: Manispaa za Angola

Angola imegawiwa katika mikoa 18 (províncias) na manispaa 158 (municípios).
Mikoa ni:

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi ni Waafrika, hasa wa makabila ya Waovimbundu (37%), Waambundu (25%) na Wakongo (13%). Machotara ni 2%, Wachina 1,4% na Wazungu 1%.

Ingawa lugha za Kibantu zinaongoza, na 6 kati yake zina hadhi ya lugha ya taifa, lugha rasmi ni Kireno.

Upande wa dini, inakadiriwa kuwa zaidi ya nusu ni Wakatoliki na robo ni Waprotestanti wa madhehebu mia tofauti.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali[hariri | hariri chanzo]

Habari[hariri | hariri chanzo]

  • allAfrica - Angola - viungo via habari
  • Angola Press -idara ya Taarifa na habari ya Angola (kwa kireno, kifaransa na kingereza)
  • Angonoticias (kwa kireno) -lango la habari lenye sifa Angola
  • Mangole (kwa kireno) - ya habari nchini Angola na pia maelekezo ya makala kwa kompyuta.
  • Jornal de Angola (kwa kireno) - Gazeti lenye sifa Angola

Maoni[hariri | hariri chanzo]

Radio na Muziki[hariri | hariri chanzo]

Maelekezo[hariri | hariri chanzo]

Utalii[hariri | hariri chanzo]

Mambo mengine[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Angola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.