Ureno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wareno)
Jamhuri ya Ureno
República Portuguesa
Bendera ya Ureno Nembo ya Ureno
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: (hakuna)
Wimbo wa taifa: A Portuguesa
Lokeshen ya Ureno
Mji mkuu Lisbon (Lisboa)
38°42′ N 9°11′ W
Mji mkubwa nchini Lisbon
Lugha rasmi Kireno1
Serikali Jamhuri
Marcelo Rebelo de Sousa
António Costa
Formation
Uhuru
24. Juni 1128
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
92,391 km² (ya 111th)
0.5%
Idadi ya watu
 - Julai 2014 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
10,427,301 (ya 83)
10,562,178
115/km² (ya 97)
Fedha Euro (€)2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
WET3 (UTC)
EST (UTC+1)
Intaneti TLD .pt
Kodi ya simu +351

-

1Kimiranda imetambuliwa kama lugha rasmi katika eneo ndogo la Ureno ya kaskazini (sheria N.º 7/99).
2Hadi 1999: Escudo ya Ureno
3Azori: UTC-1; UTC in summer


Ureno (kwa Kireno Portugal) ni nchi kwenye pembe ya kusini magharibi kabisa ya Ulaya. Upande wa magharibi na kusini imepakana na Bahari ya Atlantiki, na upande wa mashariki na kaskazini imepakana na Hispania.

Mafunguvisiwa ya Atlantiki ni pia sehemu za Ureno. Visiwa hivyo ni Azori kati ya Ulaya na Amerika na Visiwa vya Madeira vilivyoko katika sehemu ya Afrika ya Atlantiki.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina la nchi katika Kiswahili limetokana na neno la Kireno "o reino" linalomaanisha "ufalme". Wasafiri na wapelelezi Wareno kama Vasco da Gama walijitambulisha kama wawakilishi wa "Reino de Portugal" (ufalme wa Ureno). Ni sehemu ya kwanza tu iliyoingia katika lugha ya Kiswahili.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Umbo la Ureno ni kanda lenye upana wa kilomita 150 na urefu wa kilomita 475 upande wa magharibi wa Rasi ya Iberia. Mpaka na Hispania una urefu wa km 1,214 na pwani ya Atlantiki huwa na km 1,793.

Kuna sehemu mbili tofauti; hizi ni nchi upande wa kaskazini kwa mto Tejo na sehemu ya kusini. Kaskazini ina milima mingi ikiwa na tambarare katikati inayofaa kwa kilimo. Kusini kwa jumla ni tambarare pamoja na vilimavilima.

Hali ya hewa ya kaskazini ni baridi kiasi na kuna mvua nyingi lakini kusini ni joto na pakavu.

Mlima mkubwa ni Torre wenye kimo cha mita 1,993.

Mito muhimu ni Tejo, Douro (kwa Kihispania Duero) na Mondego ambayo ni mto mrefu uliopo ndani ya Ureno pekee wakati mito mingi ina chanzo katika Hispania.

Bonde la Tejo ni kitovu muhimu cha kilimo.

Kusini iko eneo la Algarve lililokuwa lengo la watalii wengi kutoka pande zote za Ulaya.

Ureno una pia mafunguvisiwa mawili katika Atlantiki mbali na bara; hayo ni Madeira na Azori. Visiwa hivi ni sehemu ya Mgongo kati wa Atlantiki viko karibu zaidi na Afrika kuliko Ureno bara.

Mlima mrefu kabisa wa Ureno ni Ponta do Pico kwenye Azori.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya kale[hariri | hariri chanzo]

Katika karne za KK Ureno ilikaliwa na makabila yaleyale ya Wakelti kama Hispania.

Waroma walitaja eneo lote la Ureno na Hispania ya leo kwa jina la "Iberia".

Tangu mwaka 450 KK sehemu za nchi zilitawaliwa na Wafinisia wa Karthago, na baada ya mwaka 200 KK yote ikawa sehemu ya Dola la Roma.

Baada ya kuporomoka ya Dola hilo mnamo 470 BK makabila ya wahamiaji wa Kigermanik walikuwa mabwana wa eneo lote.

Tangu mwaka 711 Waarabu walivamia nchi na kuitawala.

Vita vya kuwaondoa tena viliendelea kwa karne kadhaa.

Uhuru[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1143 mtawala wa eneo la mji wa Kale katika kaskazini alikuwa na uwezo wa kutosha kujitetea dhidi ya Waarabu na pia dhidi ya majirani wa eneo la Kihispania.

Baada ya ushindi katika vita dhidi ya Wahispania mwaka 1128 Afonso I alijitangaza kuwa mtawala wa kujitegemea na baadaye alichukua cheo cha mfalme. Alitumia jina la mji Kale iliyojulikana kama "Porto Kale" (bandari ya mji wa Kale) iliyokuwa "Portokale" na baadaye "Portogale".

Nchi hii ndogo ilifaulu kutunza uhuru wake hata baada ya maeneo yote mengine ya jirani kuunganishwa katika ufalme mpya wa Hispania.

Nchi hii ndogo ilikuwa kati ya nchi muhimu zaidi duniani kwa karne mbili za 15 na 16. Wafalme wake walilenga jitihada na nguvu za nchi kwa teknolojia za usafiri baharini.

Wareno waliweza kuboresha jahazi zao hadi kupita nchi zote za dunia na kwa muda wakafaulu kwenda mbali.

Wareno waligundua njia ya kuvuka rasi ya Afrika Kusini na kufika kwenye bandari za Afrika ya Mashariki hata Bara Hindi.

Ureno ilitajirika kutokana na biashara kati ya India, Asia na Ulaya. Wareno walijenga vituo kama vile maboma ya Msumbiji na Mombasa (Kenya) wakiwa mabwana wa pwani ya Afrika ya Mashariki.

Lakini nguvu za nchi ndogo hazikuweza kutetea haya yote. Baada ya kujitokeza kwa mataifa mengine kama vile Uturuki, Uholanzi, Uingereza na Ufaransa, Wareno walipaswa kuwaachia maeneo mengi.

Kati ya makoloni ya Ureno yalibaki hasa Msumbiji, Angola, Guinea Bisau, Cabo Verde, São Tomé na Príncipe katika Afrika, Brazil katika Amerika ya Kusini (hadi 1822) pamoja na maeneo madogomadogo kama Goa kwenye Bara Hindi, Timor ya Mashariki katika funguvisiwa ya Indonesia, mji wa Makao katika Uchina.

Jamhuri[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1910 Ureno iliona mapinduzi ikawa jamhuri.

Tangu 1926 hadi 1974 ilikuwa na serikali za kidikteta.

Baada ya mapinduzi ya 1974 Ureno iliacha makoloni yake yaliyobaki isipokuwa Makao kwa sababu Uchina haukuwa tayari kuipokea hadi 1999.

Ureno ikajiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1986 ikaona tena maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kireno, ambayo ni kati ya lugha za Kirumi.

Wananchi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (81%). 3.3% ni Waprotestanti. 6.8% hawana dini yoyote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Biashara
Utalii

Coordinates: 38°42′N 9°11′W / 38.700°N 9.183°W / 38.700; -9.183

Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ureno bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ureno kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.