Mgongo kati wa Atlantiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya mgongo kati ya Atlantiki

Mgongo kati wa Atlantiki ni safu ya milima chini ya maji ya Atlantiki inayoelekea kutoka 87°N (333 km kusini ya Ncha ya kaskazini) hadi kisiwa cha Bouvet katika kusini ya dunia kwenye 54°S.

Vilele vya juu vya milima hii inaonekana juu ya UB kama visiwa. Safu hii ya milima imetokea mahali ambako mabamba ya gandunia yanaachana: bamba la Ulaya-Asia na bamba la Amerika ya Kaskazini katika Atlantiki ya Kaskazini halafu bamba la Amerika ya Kusini na bamba la Afrika katika Atlantiki ya Kusini.

Mabamba haya yana mwendo wa kuachana na katika nafasi kati yao magma hupanda juu inayokuwa mwamba mpya uliosababisha kutokea kwa milima ya safu.

Kutambuliwa kwa safu hii kuliweka msingi kwa nadharia ya upanuzi wa misingi ya bahari unaosababisha mwendo wa mabamba ya gandunia.

Magma inapanda juu penye kuachana kwa mabamba ya gandunia na kujenga safu za milima ya migongo chini ya bahari

Visiwa vya mgongo kati wa Atlantiki[hariri | hariri chanzo]

Visiwa ambavyo ni vilele vya milima ya mgongo huu ni kama vifuatavyo (katika mabano ni majina ya vilele vya juu na kimo):

Nusudunia ya kaskazini (Atlantiki ya Kaskazini):

 1. Jan Mayen (Beerenberg, 2277 m)
 2. Iceland (Hvannadalshnúkur in the Vatnajökull, 2,109.6 m )
 3. Azori (Ponta do Pico au Pico Alto kwenye kisiwa cha Pico, 2,351 m
 4. Bermuda (Town Hill kwenye kisiwa cha Main Island, 76 m)
  (Bermuda ilianzishwa juu ya mgongo lakini imesogea mbali sasa)
 5. Saint Peter and Paul Rocks (Southwest Rock, 22.5 m)

Nusudunia ya kusini (Atlantiki ya Kusini):

 1. Kisiwa cha Ascension (The Peak, Green Mountain, 859 m)
 2. Tristan da Cunha (Queen Mary's Peak, 2062 m)
 3. Kisiwa cha Gough (Edinburgh Peak, 909 m)
 4. Kisiwa cha Bouvet (Olavtoppen, 780 m)