Nenda kwa yaliyomo

Azori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Região Autónoma dos Açores
Jimbo la kujitawala la Azori
Bendera ya Azori Nembo ya Azori
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Antes morrer livres que em paz sujeitos
(Heri kufa huru kuliko amani ya utumwa)
Wimbo wa taifa: A Portuguesa (kitaifa)
Hino dos Açores (kijimbo)
Lokeshen ya Azori
Mji mkuu Ponta Delgada (Serikali ya kijimbo)
Angra do Heroísmo (mahakama kuu)1
Horta (Bunge la Jimbo)2
37°44′ N 25°40′ W
Mji mkubwa nchini Ponta Delgada
Lugha rasmi Kireno
Serikali
Rais
Jimbo la kujitawala
Vasco Cordeiro
Kukaliwa na watu
Jimbo la kujitawala

1976
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2,333 km² ( )
Idadi ya watu
 - 2001 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
241,763 ( )
104/km² ( )
Fedha Euro (€)3 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
UTC-1 (UTC)
UTC in EST (UTC)
Intaneti TLD .pt
Kodi ya simu +351

-

1Angra do Heroísmo: 38º 39' N 27º 13' W
2Horta: 38º 32' N 28º 38' W
3Kabla ya 2002: Escudo ya UrenoAzori (kwa Kireno: Ilhas dos Açores - Visiwa vya vipanga) ni funguvisiwa la Ureno lenye visiwa tisa vikubwa na vingine vidogo katika Atlantiki takriban km 1,500 magharibi ya Ulaya na 3,600 mashariki ya Amerika ya Kaskazini.

Ni jimbo la kujitawala la Ureno (Região Autónoma dos Açores) na sehemu ya Umoja wa Ulaya.

Visiwa vyote ni vya asili ya kivolkeno; hali halisi ni vilele vya milima mirefu sana vinavyotoka nje ya maji kutoka sakafu ya bahari. Milima hiyo ni sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki yanapokutana mabamba ya gandunia ya Amerika ya Kaskazini na Afrika.

Mlima Pico kwenye kisiwa cha Pico ni mlima mrefu wa Ureno wenye kimo cha m 2,351 juu ya UB.

Visiwa viligunduliwa na mabaharia Wareno mwaka 1427: vilipatikana bila wanadamu. Wakazi wa kwanza walifika kutoka Ureno mwaka 1439.

Visiwa vikubwa zaidi vya funguvisiwa la Azori
Kisiwa Eneo
(km²)
São Miguel 759
Pico 446
Terceira 403
São Jorge 246
Faial 173
Flores 143
Santa Maria 97
Graciosa 62
Corvo 17

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Azori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.