Svalbard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Svalbard.

Svalbard ni jina la funguvisiwa la Norwei katika Bahari ya Aktika, linalojulikana pia kama funguvisiwa la Spitsbergen.

Iko kati ya Norwei na ncha ya kaskazini ya dunia.

Kuna wakazi 2,756 kwenye visiwa vitatu vya Spitsbergen, Bjørnøya (Kisiwa cha Dubu) na Hopen. Makao makuu ni kijiji cha Longyearbyen.

Mkataba wa kimataifa wa Svalbard umekubali ya kwamba funguvisiwa liko chini ya Norwei lakini kuna masharti fulani. Raia wa nchi zote 40 zilizotia sahihi mkataba huo wana haki ya kuingia huko na kufanya shughuli zao. Hivyo kuna kijiji cha Kirusi cha Barentsburg ambako Warusi wanachimba madini.

Kisiwa cha Dubu (Bjørnøya byornoya, kwa Kiingereza: Bear Island) hutazamwa kama sehemu ya kusini kabisa ya Svalbard, ingawa ni kisiwa cha pekee chenye umbali wa km 235 kutoka Spitsbergen.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Svalbard kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.