Spitsbergen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa Spitsbergen
Spitzbergen kutoka satelaiti wakati wa joto (mwezi wa Julai: peupe ni barafu)

Spitsbergen (pia: Spitzbergen) ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa vya Svalbard inayoitwa mara nyingi wa jina Spitsbergen vilevile kwa jumla. Iko ndani ya Bahari ya Aktiki na eneo lake ni 39,044 km². Funguvisiwa yote ni sehemu ya ufalme wa Norwei.

Mwiinuko mkuu ni mlima wa Newtontoppen mwenye kimo cha mita 1717.

Wakazi wa kisiwa ni Wanorwei na Warusi kwa jumla hawazidi watu 2100.

Biashara ya kisiwa ni utalii na migodi pekee; hakuna kilimo kutokana na baridi. Mimea hustawi katika wiki chache za joto kidogo na hii inatokea kwenye asilimia 10 ya eneo la kisiwa pekee, maeneo mengine ni baridi mno.

Kuna mji mmoja ambao ni Longyearbyen mwenye wakazi 1700. Mji mdogo wa pili ni Barentszburg inayokaliwa na Warusi 400 wanaozidi upungua. Mji wa Pyramiden ilikuwa kituo kikubwa cha kuchimba makaa lakini haina watu tena tangu mwaka 2000.

Spitsbergen haina wenyeji asilia. Visiwa vilitembelewa na wavuwi tu waliovinda hapa nyangumi wengi. Tangu karne ya 18 walikuwepo wavindaji wachache waliojenga vibanda na kukaa hapa kwa muda wa miaka lakini hapakuwa na wakazi wa kudumu kabisa.

Mnamo mwaka 1900 makaa yaligunduliwa kwa wingi na sasa makazi ya kwanza ya kudumu kwa ajili ya wafanyakazi yalijengwa. Kwa njia hii mji wa Longyearbyen ulianzishwa tangu mwaka 1906. Hadi wakati ule hakuna nchi iliyokuwa na mamlaka juu ya visiwa.

Mnamo 1920 nchi za Norwei, Denmark, Ufaransa, Italia, Japani, Uswidi, Marekani na Ufalme wa Maungano (Uingereza) zilikubaliana masharti ya mkataba wa Spitsbergen. Masharti mawili muhimu ni ya kwamba

  1. funguvisiwa itakuwa chini ya mamlaka ya Norwei
  2. nchi zote zinazotia sahihi kwenye mkataba huu zina haki ya kuwa na shuguli za kiuchumi kwenye visiwa.

Nchi nyingine zilijiunganisha na mkataba baadaye. Lakini ni Norwei na Urusi pekee ambazo zina shughuli wenye visiwa hivi. Wakati wa Umoja wa Kisovyeti walikuwepo Warusi wengi hapa waliochimba makaa na madini mengine lakini migodi yote haileti faida tena imefungwa kwa kiasi kikubwa.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: