Jina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Jina ni neno au maneno ambayo wanapewa watu, wanyama, nchi, vitu n.k. kwa ajili ya utambulisho.

Majina ya watu[hariri | hariri chanzo]

Utamaduni, kwa njia ya sheria au desturi, ndio unaoratibu namna ya kupanga na kutumia majina ya watu, kwa kawaida tangu kuzaliwa.

Mara nyingi, pamoja na jina binafsi, mtu anatumia pia majina mengine kama vile la ukoo mzima, au la baba na la babu.

Katika nchi na makabila mbalimbali jina linaweza kubadilishwa, kwa mfano wakati wa ibada wa kuingizwa katika dini fulani, au kuongezewa, kwa mfano kutokana na ndoa.

Mara nyingine jina linafupishwa, hasa kama ni refu mno, au linapambwa kama kwa kumbembeleza mwenye nalo.