Ndoa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Pete, mfano wa ndoa

Ndoa ni muungano wa maisha yote kati ya watu wawili unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii.

Katika utamaduni wa nchi nyingi uhusiano huo ni kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja tu na unalenga ustawi wao na uzazi wa watoto katika familia.

Katika nchi nyingine inakubalika ndoa kati ya watu wawili ambao mmojawao ana au anaweza kuwa na mwenzi au wenzi wengine pia (mitara), hususan ndoa ya mwanamume mmoja na wanawake zaidi ya mmoja. Kumbe kwingine hilo ni kosa la jinai.

Miaka ya mwisho nchi chache zimeanza kuruhusu ndoa kati ya watu wawili wa jinsia moja. Kumbe nchi nyingine zinapinga vikali jaribio hilo kama kinyume cha maumbile. Takwimu zinaonyesha kwamba katika ndoa za jinsia moja uaminifu ni mdogo kuliko katika ndoa za jinsia mbili, na kwamba udumifu wake ni wa muda mfupi zaidi.

Mara nyingi harusi inafanyika kwa ibada maalumu kadiri ya dini ya wahusika.

Baadhi ya madhehebu ya Kikristo yanatazama ndoa kati ya wabatizwa wawili kuwa sakramenti: rejea Ndoa (sakramenti). Hasa Kanisa Katoliki linaamini ndoa haiwezi kuvunjwa kwa talaka.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndoa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.