Nenda kwa yaliyomo

Ndoa ya jinsia moja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ndoa za jinsia moja)
     Nchi ambazo huruhusu harusi za jinsia moja      Nchi zinazotambua ndoa za wapenzi wa jinsia moja iliyofanywa mahali pengine      Nchi hizi huruhusu makubaliano yanayofanana na ndoa      Nchi hizi hazitambui makubaliano ya wapenzi wa jinsia moja

Ndoa za jinsia moja ni makubaliano kati ya wanaume wawili au wanawake wawili ili kuishi pamoja kwa mfano wa mume na mke.

Ndoa ya namna hiyo ni halali katika nchi zaidi ya ishirini duniani. Nchi hizo (kwa mwaka wa 2019, na kwa mpangilio wa muda wa idhini) ni: Uholanzi, Ubelgiji, Uhispania, Kanada, Afrika Kusini, Norwei, Uswidi, Ureno, Aisilandi, Ajentina, Denimaki, Brazil, Ufaransa, Uruguay, Nyuzilandi, Uingereza na Welisi, Uskoti, Luxemburg, Marekani, Eire, Grinilandi, Kolombia, Ufini, Visiwa vya Faroe, Malta, Ujerumani, Australia, Austria, Taiwan na Ekuador.

Majimbo mengi huko Mexiko pia huruhusu ndoa ya jinsia moja. Majimbo yote katika Mexico lazima yatambue ndoa hizi.

Israeli inatambua ndoa zilizofanywa nje ya nchi.

Sheria itapaswa kubadilishwa huko Eire ya Kaskazini na Kosta Rika. Huko Panama pia walisema watahalalisha ndoa ya jinsia moja. Mahakama ya Amerika Nzima ya Haki za Binadamu imeamua kuhalalisha ndoa ya jinsia moja. Uamuzi wake ni wa lazima kwa nchi zote za Amerika ya Kilatini isipokuwa kwa Venezuela na Kuba, lakini nchi zote mbili zinajadili kuhalalishwa bila kujali.

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu imeonyesha kwamba korti hiyo iko tayari kutangaza ndoa ya jinsia moja haki za binadamu mara nchi za kutosha zitakapoihalalisha.

Pia kumekuwa na mazungumzo juu ya kuhalalisha ndoa kama hizo katika nchi za Asia kama Ufilipino, Uthai, Kamboja, Nepali na Japani. Singapuri, Hong Kong na Beijing hutoa haki za kuishi kwa wanandoa wa jinsia moja wa kigeni, lakini haitoi ruhusa ya kuunda vyama kama hivyo kwa raia zao.

Nchi nyingine nyingi, hasa za Afrika na za Kiislamu, hazikubali mahusiano ya namna hiyo kwa kuyaona ni kinyume che maumbile ya watu na tabia ya ndoa kuhusiana na uzazi. Hivyo wanapinga kwamba hii ni haki ya binadamu.

Kwa msingi huohuo nchi kadhaa zinaruhusu makubaliano yanayofanana na ndoa lakini hayaitwi "ndoa". Hizi (kwa herufi ya alfabeti) ni Andorra, Aruba, Chile, Eire ya Kaskazini, Estonia, Hungaria, Italia, Kroatia, Kupro, Liechtenstein, San Marino, Slovenia, Ucheki, Ugiriki na Uswisi.

Suala likoje

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 2000 idadi inayozidi kuongezeka ya nchi zimeanza kuruhusu ndoa kati ya watu wawili wa jinsia moja. Kumbe nchi nyingine zinapinga vikali jaribio hilo kama kinyume cha dini na desturi au hata maumbile yenyewe.

Tabia za kingono kati ya wanyama wa jinsia moja zimeonekana katika spishi 500 hivi duniani kote,[1][2] lakini wanaosema kuwa ushoga ni kinyume cha maumbile wanamaanisha maumbile ya binadamu yanayotakiwa kuongozwa na akili na utashi, si silika tu kama ilivyo kwa viumbehai wengine wote. Kwa mfano, ubakaji unafanywa na wanyama mbalimbali, lakini kwa binadamu haufai kabisa.

Takwimu zinaonyesha kwamba katika ndoa za jinsia moja uaminifu wa moyoni na wa mwilini ni mdogo kuliko katika ndoa za jinsia mbili.[3] Pia "Idara ya Haki" ya Marekani imeripoti matukio ya ukatili mengi sana katika jozi za jinsia moja kuliko ya zile za jinsia mbili[4] kama ilivyowahi kuonyeshwa na utafiti wa Chuo Kikuu cha Michigan [5]

Uchunguzi mwingi umeonyesha kwamba wanaume waliofunga ndoa za jinsia moja wana kiwango cha talaka cha chini kidogo kikilinganishwa na kile cha watu waliofunga ndoa za jinsia mbili[6][7] na zile za wanawake wawili.[8][9]

Kiwango cha juu cha talaka kati ya wanawake kinapatana na takwimu zinazoonyesha kwamba kwa ujumla wanawake ndio wanaoanzisha talaka zilizo nyingi.[10][11]

  1. Bagemihl, Bruce (1999). Biological Exuberance: Animal Homosexuality and Natural Diversity. St. Martin's Press. ISBN 978-0-312-25377-6.
  2. Harrold, Max (1999-02-16). "Biological Exuberance: Animal Homosexuality and Natural Diversity". The Advocate, reprinted in Highbeam Encyclopedia. Iliwekwa mnamo 2007-09-10.
  3. Symons suggests that all men are innately disposed to want sexual variation and that the difference between heterosexual and homosexual men is that homosexual men can find willing partners more often for casual sex, and thus satisfy this innate desire for sexual variety. Harris, C. R. (2002). "Sexual and romantic jealousy in heterosexual and homosexual adults". Psychological Science. 13 (1): 7–12. doi:10.1111/1467-9280.00402. PMID 11892782.
  4. https://bjs.ojp.gov/content/pub/pdf/vvsogi1720.pdf
  5. https://www.lifesitenews.com/news/study-almost-half-of-gay-men-abused-by-their-partners/
  6. Marian Jones (1 Mei 1997). "Lessons from a Gay Marriage: Despite stereotypes of gay relationships as short-lived, gay unions highlight the keys to success". Psychology Today. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Andersson, Gunnar (Februari 2006). "The Demographics of Same-Sex 'Marriages' in Norway and Sweden" (PDF). Demography. 43 (1): 79–98. doi:10.1353/dem.2006.0001. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2009-03-25. Iliwekwa mnamo 2019-07-24. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. EL. "Marital Bliss? Gender Gaps..." Gender Across Borders. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-27. Iliwekwa mnamo 26 Desemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. https://www.lifesitenews.com/blogs/skyrocketing-lesbian-divorce-rates-show-failure-of-same-sex-couples-imitating-marriage
  10. In the Netherlands of the 580 lesbian couples who were married in 2005, 30% were divorced ten years later compared to 18% for heterosexual couples and 15% for gay male couples. Janene Pieters (1 Machi 2016). "Marriages Between Women Most Likely To End In Divorce". NL Times. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. Marian Jones (1 Mei 1997). "Lessons from a Gay Marriage: Despite stereotypes of gay relationships as short-lived, gay unions highlight the keys to success". Psychology Today. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndoa ya jinsia moja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndoa ya jinsia moja kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.