Ufilipino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Repúbliká ng̃ Pilipinas
Jamhuri ya Ufilipino
Bendera ya Ufilipino Nembo ya Ufilipino
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Maka-Diyos, Makatao, Makakalikasan, at Makabansa
("Kwa Mungu, watu, mazingira na nchi")
Wimbo wa taifa: Lupang Hinirang ("Nchi teule")
Lokeshen ya Ufilipino
Mji mkuu Manila
14°35′ N 121°0′ E
Mji mkubwa nchini Quezon City
Lugha rasmi Kifilipino na Kiingereza*
Serikali Jamhuri
Benigno Aquino III
Jejomar Binay
Uhuru
Ilitangazwa
kujitawala
Ilitambuliwa
Katiba

12 Juni 1898
24 Machi 1934
4 Julai 1946
2 Februari 1987
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
300,000 km² (ya 72)
0.6
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
85,236,913[1] (ya 12)
76,504,077
276/km² (ya 42)
Fedha Philippine peso (piso) (PHP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
PST (UTC+8)
(UTC)
Intaneti TLD .ph
Kodi ya simu +63
* Kicebuano, Kiilokano, Kihiligaynon, Kibikol, Kiwaray-waray, Likapampangan, Kipangasinan, Kinaray-a , Kimaranao , Kimaguindanao, Kitagalog, Kitausug ni lugha rasmi kieneo. Kihispania na Kiarabu hutambuliwa kwa msingi wa matumizi ya hiari.Ufilipino (Kifilipino : Pilipinas), ni nchi ya kisiwani kwenye Funguvisiwa ya Malay katika Asia ya Kusini-Mashariki. Mji mkuu ni Manila. Ina visiwa 7,107 vyenye eneo la 300,000 km².

Nchi iliitwa kwa jina la Kihispania "Las Islas Filipinas" (Visiwa vya Filipo) na Ruy López de Villalobos kwa heshima ya mfalme Filipo II wa Hispania. Hispania ilitwala eneo tangu 1565 hadi Mapinduzi ya Ufilipino wa 1896. Marekani ilitwaa visiwa 1898 katika vita ya Vita ya Marekani dhidi Hispania na kuvitawala kama koloni hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia wakati Japani ikatwaa nchi kwa miaka minne.

Baada ya vita Ufilipino ikapewa uhuru wake.

Wakazi wengi wa Ufilipino hufuata Ukristo wa Kikatoliki (zaidi ya 80%) ambao ni urithi wa athira ya Kihispania. Lugha ya Kiingereza iliachwa na Marekani kama lugha rasmi pamoja na Kifilipino; pia kuna lugha nyingi za asili (angalia orodha ya lugha za Ufilipino). Athira ya Kiislamu huonekana hasa kwenye kusini ya kisiwa cha Mindanao kwa jumla 5% za Wafilipino ni Waislamu wa dhehebu la Sunni.

Siasa na serikali[hariri | hariri chanzo]

Ufilipino ina serikali ya urais, tena ya umoja (na tofauti kiasi sababu baadhi ya maeneo yana uhuru mkubwa kutoka serikali ya kitaifa) ambapo Rais ni mkuu wa nchi na kiongozi wa serikali na pia ni kamanda mkuu wa majeshi. Rais huchaguliwa kwa kura ya umma kwa kipindi kimoja cha miaka sita, wakati ambapo yeye huteua na kusimamia baraza la mawaziri. [2] Kongamano la bunge limeundwa na Seneti, inayohudumu kama jumba kuu linalo wajumbe waliochaguliwa kwa muda wa miaka sita, na Baraza la Wawakilishi, inayohudumu kama jumba ndogo, inayo wajumbe waliochaguliwa kwa muda wa miaka mitatu. Wao huchaguliwa kutoka kwa wilaya za bunge na kupitia sekta za uwakilishi. [2] Nguvu za kimahakama zimewekwa katika Mahakama Tukufuiliyoundwa na Jaji Mkuu kama afisa msimamizi, na majaji washirikishi kumi na Wanne wote walioteuliwa na Rais kutoka mapendekezo ya Baraza la Mahakama na Korti. [2] Kumekuwa majaribio kubadilisha serikali iwe shirikisho, ya bunge moja au serikali ubunge mwanzo katika muda wa Ramos hadi sasa. [48] [49]

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kuna mikoa ifuatayo:

Geography of the Philippines

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ufilipino ina visiwa 7,107 vinavyohesabiwa katika kundi tatu zinazoitwa kufuatana na kuwa karibu na visiwa vikubwa vya:

Luzon ni kisiwa kikubwa na Mindanao ni kisiwa cha pili. Visaya ni kundi la visiwa katikati ya funguvisiwa. Mji mkuu wa Manila uko Luzon. Quezon City ni mji mkubwa. Cebu City ni mjimkubwa upande wa Visaya. Davao City ni mji mkuu wa Mindanao.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Tovuti rasmi[hariri | hariri chanzo]

Ona Pia[hariri | hariri chanzo]

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufilipino kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.