Mke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bibiarusi wa Indonesia.
Sehemu nyingi pete ni ishara mojawapo ya mtu kuwa na ndoa.

Mke ni binadamu wa jinsia ya kike ambaye ameoana na mwanamume.

Katika adhimisho la ndoa, mwanamke anaitwa pia bibi arusi.

Mwanamke wa namna hiyo anaendelea kuitwa mke hadi ndoa ivunjike kwa kifo cha mumewe (hapo ataanza kuitwa "mjane") au kwa talaka (hapo ataanza kuitwa "mtaliki").

Utengano haumuondolei hadhi ya kuwa mke wala haki zinazoendana nayo kadiri ya sheria na desturi za jamii husika.

Katika tamaduni kadhaa, ndoa inatazamiwa kwa ujumla kwamba mwanamke achukue jina la ukoo la mume wake, ingawa hilo si la kawaida. Mwanamke aliyeolewa anaweza kuonyesha hali yake ya ndoa kwa njia kadhaa; katika tamaduni za Magharibi, mwanamke aliyeolewa kwa kawaida huvaa pete ya ndoa lakini katika tamaduni nyingine, alama nyingine za hali ya ndoa zinaweza kutumika.