Jinsia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Uzazi wa kijinsia wa binadamu na wanyama wengi unafanyika kwa mbegu mojawapo kati ya nyingi zinazobebwa na manii ya mzazi wa kiume kuungana na kijiyai cha mzazi wa kike. Picha hii iliyokuzwa sana inaonyesha mbegu inayojipenyeza katika kijiyaji cha duara.

Jinsia ni hali ya viumbe hai wengi kuwa wa kiume au wa kike, jambo muhimu katika mpango wa kuendeleza uhai kupitia uzazi.

Binadamu[hariri | hariri chanzo]

Kati ya wanadamu hali ya kuwa mwanamume au mwanamke inategemea nukta ya utungaji mimba na kudumu moja kwa moja.

Inatokana na milioni za mbegu zilizomo kwa kawaida katika shahawa ya mwanamume, ambazo baadhi yake ni za kiume (zenye chembeuzi Y) na baadhi za kike chembeuzi X.

Kijiyai cha mwanamke hakichangii uainishaji wa jinsia ya mtoto, kwa kuwa kina pea ya chembeuzi X tu.

Ikiwa mbegu inayowahi kujipenyeza katika kijiyai cha mwanamke ni ya kiume, mimba itakuwa ya kiume (XY), kumbe ikiwahi moja ya kike, mimba itakuwa ya kike (XX).

Kulingana na tofauti hiyo, binadamu huyo mpya atazidi kukua na kutokeza viungo maalumu vya uzazi kama:

Viungo hivyo vitakomaa wakati wa ubalehe.

Ni pia muhimu kazi ya chachu za jinsia (homoni za jinsia) zilizo tofauti kwa mwanamume na mwanamke.

Sehemu fulani ya tofauti kati ya jinsia mbili hutegemea pia utamaduni.

Hali za watu zisizo za kawaida[hariri | hariri chanzo]

Katika kila jamii, hasa zilizoendelea, kuna idadi fulani ya watu ambao utambuzi wa jinsia si wa kawaida kutokana na hali ya pekee ya chembeuzi (hasa XYY na XXY) au uwepo wa homoni za jinsia nyingine ndani yao au uwepo wa viungo vya uzazi mchanganyiko au visivyo kamili au visivyoeleweka. Hata hivyo chembeuzi Y inathibitisha kuwa mhusika ni wa kiume.

Watu wengine wana tatizo la utasa, ambalo linazidi kuongezeka hasa katika nchi zilizoendelea hata kuvuka asilimia 10 ya wakazi.

Wengine, kwa sababu zisizoelezeka vya kutosha na biolojia wala saikolojia, hawajisikii ipasavyo na jinsia yao (hasa ubaridi wa kijinsia na elekeo la ushoga na usagaji).

Viumbe hai visivyozaliana kijinsia[hariri | hariri chanzo]

Si viumbe vyote vinavyoendeleza uhai kwa njia ya uzaliano kijinsia;

Kuna pia njia ya kujizalisha ambayo ni namna ya pekee ya uzalioni kijinsia. Mimea kama karanga na pia wanyama kadhaa mfano vyawa na samaki kadhaa wanaweza kuanzisha wadogo bila manii ya kiume. Wanyama kama mategu ni huntha wanaobeba manii pamoja na vijiyai mwilini na wanazaa ndani yao.