Karanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Karanga (Moshi Mjini)

Karanga zilizokauka

Karanga au njugu ni matunda la mnjugu na kati ya mazao muhimu duniani. Vikonyo vya karanga vinaingia katika ardhi na makaka yanaiva hapa chine. Baada ya kukauka makaka haya na matunda ndani yao hufanana na jozi kwa hiyo kuna majina kama "jozi ya ardhini" katika lugha mbalimbali[1] .

Karanga zinaliwa moja kwa moja hasa baada ya kukaangwa, zinasagwa kuwa siyagi ya karanga na hasahasa zinasagwa na kukandamizwa kwa kupata mafuta ya karanga kwa upishi au matumizi viwandani. Mabaki ya karanga baada ya kutolewa kwa mafuta ni lishe bora la nyongeza kwa mifugo kama ng'ombe.

Karanga au mafuta yake zinaweza kusababisha mzio kwa asilimia mdogo wa watu lakini hii ni tatizo katika nchi ambako chakula ni hasa chakula kilichopandaliwa viwandani kutokana na matumizi mapana ya karanga.

Marejeo=[hariri | hariri chanzo]

  1. ing. groundnut, jer. Erdnuss, hol. aardnoot, far. بادام زمینی badam zamini, lakini Kiafrikaans grondboontjie "maharagwe ya ardhini"