Mzio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mzio (kwa Kiingereza: allergy) hutokea pindi mwili wa mwathirika unapokumbana na vitu hewani ambavyo haviwadhuru walio wengi. Vitu hivyo vinahusisha chavua, au chakula fulani ambacho kwa watu wengine hakileti madhara yoyote. Mfumo wa kinga mwilini mwako huzalisha kingamwili.

Ikiwa mzio utazuka, mfumo wa kinga mwilini mwako huutengeneza kingamwili ambazo kazi yake ni kubaini vizio vyote hata kama si hatarishi. Ikiwa utakaribiana na vizio, mfumo wa kinga utafanya mwili wako kuwasha, pua kuchochota, njia ya hewa na mfumo wa mmeng’enyo kuashiriria hitilafu katika mwili.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzio kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.