Mchanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maji na mchanga mwambaoni

Mchanga ni punje ndogo za mwamba uliosagwa.

Kufuatana na mapatano ya kitaalamu mawe huitwa "mchanga" kama punje zake ziko kati ya milimita 0.063 hadi 2.

Punje hizi zatokana na mmomonyoko wa mawe makubwa zaidi kama changarawe yaliyosukumwa na upepo au maji kwa mfano mtoni, baharini au kwenye mteremko wa mlima.

Mchanga hupatikana kwa wingi hasa kando ya bahari, jangwani au mtoni.

Mchanga ukichanganywa na saruji na maji huwa zege inayotumiwa kwa ujenzi.

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mchanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.