Saruji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kiwanda cha saruji
Picha:Orange cement mixer.jpg
Machine ndogo cha kukoroga saruji, maji na machanga

Saruji (pia: simiti, simenti) ni mata laini kama ungaunga unaotengenezwa kutokana na chokaa, udongo wa ufinyanzi, mchanga, chuma na mengine. Kwa kawaida huonekana kama unga wa rangi ya kijivu.

Hukorogwa na maji kuwa na hali kati ya ujiuji baada ya muda inaanza kuganda na kuwa imara kama jiwe.

Saruji imekuwa muhimu sana katika shughuli za ujenzi. Awali ilitumiwa kwa kushika mawe au matofali ya ukuta vikae pamoja.

Baadaye ikagunduliwa ya kwamba saruji ikichanganywa na mchanga kuwa zege inaweza kumwagwa kati ya bao mbili na kuwa imara ndani yao. Kwa njia hiyo imewezekana kujenga haraka sana kwa kumwaga mchanganyiko wa zege ya saruji katika nafasi zilizoandaliwa awali. Hapa vyuma vinaingizwa ndani ya ukuta au sakafu ya saruji kwa kusudi la kuongeza uimara.

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: