Teknolojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Katika nusu ya pili ya karne ya 20 wanadamu walifaulu kutumia teknolojia mbalimbali kuwafikisha watu kwenye anga la nje.

Teknolojia ni elimu inayohusu uhandisi, ufundi, ujenzi, vifaa na mbinu za uzalishaji wa vifaa na huduma katika jamii.

Asili ya neno ni Kigiriki "τέχνη" (tamka: tékhne): „uwezo, usanii, ufundi".

Teknolojia inaweza kumaanisha:

  • vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu
  • elimu ya matumizi yake pamoja na mbinu na maarifa jinsi ya kutumia sayansi
  • uwezo wa kubadili malighafi asilia na kuwa bidhaa yenye thamani inayoweza kukidhi mahitaji ya binadamu. Hapa bidhaa haimaanishi tu vitu kama magodoro, magari ya kutembelea, unga wa ngano n.k., la hasha: ni huduma yoyote inayotolewa kwa jamii, mfano huduma ya usafiri, huduma ya utalii, huduma ya chakula, na pamoja na vitu vyote vinavyozalishwa viwandani.

Tazama pia