Hadubini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mtaalamu akichungulia kwenye hadubini
Hadubini ya kawaida
1:Lenzi kwa jicho cha mtazamaji
2-3 lolenzi tatu kwa kukuza
4-5 mguu na gurudumu la fokasi
6 meza ya kiolwa (kinachotazamiwa)
7-8 taa inayoangaza kiolwa kwa chini; au kioo kinachokusanya nuru chini ya kiolwa kama hakuna umeme
Jicho la inzi jinsi inavyoonekana kwa hadubini

Hadubini (pia: darubini ya vidudu) ni kifaa cha kutazama vitu vidogo sana. Ni chombo muhimu cha sayansi kwa utafiti wa vitu ambavyo ni vidogo mno kwa jicho la binadamu.

Hadubini ya kawaida (hadubini maonzi) huwa na lenzi zinazokuza kiolwa kinachowekwa chini yake. Kwa kawaida kuna lenzi kadhaa zenye viwango tofauti vya kukuza. Muundo wake hufanana na darubini lakini unaangalia vitu kwa karibu ambavyo ni vidogo kimaumbile. Darubini inaangalia violwa vya mbali vinayoonekana vidogo kutokana na umbali.

Uwezo wa hadubini ya kawaida ni kukuza hadi mara 1,500.

Kwa utafiti wa vitu vidogo zaidi kuna teknolojia ya hadubini elektronia. Kifaa hiki hutumia elektroni badala ya nuru kwa utafiti wake na kuwezesha kutazama yaliyomo ya molekuli.

Chanzo cha neno Hadubini[hariri | hariri chanzo]

Kuhusu Hadubini yafaa ielezwe kwamba neno hili la Kiswahili liliundwa mwaka 1977 na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya nchini Tanzania, (Shaikh) Jamil R. Rafiq.

Hapo kabla kulikuwa hakuna neno lolote la kueleza 'microscope' kwa Kiswahili. Kamusi zilieleza neno 'darubini' likiwa Kiswahili cha Telescope na Microscope, ilhali neno hili lamaanisha Telescope peke yake.

Sheikh Jamil R. Rafiq alipendekeza neno Hadubini kwa chombo kiitwacho microscope katika makala yake iliyotangazwa katika gazeti la Daily News la tarehe 8 Machi 1977. Wananchi wengi wakalipenda neno hili likubaliwe katika Kiswahili. Hatimaye, Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) likakubali rasmi neno hili katika Kiswahili, likaanza kutumika katika vitabu vya sayansi.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Sehemu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hadubini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.