Virusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Virusi ya aina rotavirus

Virusi (kutoka lat. virus "sumu“) ni chembe kidogo sana iliyoundwa na mada genetiki kama DNA na RNA kinachoweza kuzaa kwa msaada wa seli za viumbehai.

Wakati mwingine huhesabiwa kati ya vidubini lakini wataalamu wengi wanakataa ni viumbehai maana haiwezi kuzaa yenyewe pia haina metaboli. Si seli yenyewe lakini ina sehemu za kiini cha seli.

Virusi vinaingia katika seli ya kiumbehai kama mmea au mnyama au binadamu vikitumia seli hii hii kuzaa yaani kujizidisha mara elfu kadhaa. Tendo hili linasababisha vurugu ndani ya seli za kimelea inayoonekana kama hali ya ugonjwa.

Hadi sasa kuna aina za virusi zaidi ya 5000 zilizotambuliwa.

Virusi ni vidogo kuliko bakteria. Zimeonekana tu tangu kupatikana kwa hadubini elektronia. Muundo wa virusi una sehemu mbili pekee: uzi wa DNA au RNA halafu koti ya proteini ya kulinda uzi hiyo.

Ambukizo la virusi katika wanyama na watu husababisha mjibizo wa kingamwili unaoelekea kuua virusi. Lakini mjibizo huu unaoonekana mara nyingi kwa homa unaweza kudhoofisha mwili na kuleta hali ngumu hadi kifo.

Ni vigumu kupata madawa ya virusi kwa sababu virusi huishi ndani ya seli za mwili hivyo kuna hatari ya kwamba dawa linasababisha hasara kwa seli zenyewe.

Kati ya magonjwa yanayosababishwa na virusi ni influenza (homa ya mafua) na pia UKIMWI. Aina kadhaa za virusi zinaweza kusababisha kansa.