Kiumbehai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bakteria ya Escherichia coli ni mfano wa viumbehai katika kundi la prokariota
Sifongo ya baharini ni mfano wa viumbehai katika kundi la eukariota

Kiumbehai ni kitu kilicho hai kama vile binadamu, mnyama, mmea au bakteria. Kwa upande mmoja viumbehai ni molekuli za mata jinsi ilivyo kwa vitu vingine kwa mfano udongo, mawe, fuwele au hewa. Kwa upande mwingine mata hii ina mfumo mwenye tabia mbalimbali ambazo kwa pamoja zinaunda uhai kama vile uwezo wa kuzaa, kukua na umateboli (uwezo wa kujenga au kuvunja kemikali mwilini). Hata kama sayansi haijui kikamilifu uhai ni nini inatambua jumla ya tabia hizi kama dalili za uhai.

Kiumbehai inaweza kuwa na seli moja kama bakteria kadhaa au kuwa na seli mamilioni kama mwanadamu.

Viumbehai vyenye seli moja tu ni vidogo sana havionekani kwa jicho bali kwa hadubini tu.

Aina za viumbehai[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu wamegawa viumbehai katika vikundi vitatu kufuatana na muundo wao wa ndani:

Vikundi hivi ni domeni 3 za uainishaji wa kisayansi.

Virusi ni kitu kati ya kiumbehai na kitu kisicho hai; wataalamu wengine husema ya kwamba haistahili kuitwa "kiumbehai" kwa sababu haiwezi kuzaa pekee yake haina umetaboli wake bali unategemea kuingia ndani ya seli na kutumia nafasi za seli kwa kuzaa kwake.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiumbehai kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.