Figo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Figo ya binadamu.

Figo ni kiungo cha mwili ambacho ni cha kutatanisha: figo hufanya kazi mbalimbali muhimu katika mwili wa binadamu na wanyama wengi. Ila kazi yake kuu ni kusawazisha maji ndani ya mwili kwa kuchuja na kusitiri bidhaa za chembechembe kama vile urea na minerali katika damu na kuchuja hizo, pamoja na maji na mkojo.

Kwa maana figo zimeumbwa kuhisi ukolezi wa plazma ya ioni kama vile sodiamu, potasiamu, hidrojeni, oksijeni, hewa na msombo kama vile asidi amino, kreatini, bikaboneti na glukosi, figo husawazisha shinikizo la damu, hali ya ujenzi wa glukosi katika chembechembe, na erithropoesisi yaani maendeleo ya kazi ya kutengeneza selidamu nyekundu).

Sayansi ichunguzayo figo na maradhi ya figo inaitwa nefrolojia. Kiambishi awali "[nefro]" kimaanishacho figo kimetoka kwa lugha ya Kigiriki cha kale, "[nefros] [νεφρός]".

Utambi na kipimo chake ni sentimeta 9 mpaka 13 kwa kipenyo, kipimo cha figo la kushoto ni kikubwa kidogo kuliko cha la kulia. Yapo kwenye ukolezi wa mwiba T12 na L3.

Upande wa sehemu za juu ya figo zimehifadhiwa na ubavu wa kumi na moja na wa kumi na mbili, katika kila figo pamoja na tezi ya adrenali zimefunikwa na ngozi mbili zenye mafuta na renal fascia inayosaidia kuimarisha figo.

Watu wachache wamezaliwa na figo moja tu, hali hiyo hujulikana kama "unilateral agenesis" kwa Kiingereza, pia kuna watu wachache waliozaliwa bila figo lolote, hali hiyo inajulikana kama "bilateral agenesis".

Figo hupata damu chafu kwenye mkole wa tumbo ambayo imegawika katika matawi mawili, ateri moja kwa upande wa kulia na nyingine kwa upande wa [kushoto]. Kisha damu ambayo imeshakwisha kuchujika inarudia tena kwenye vena ya damu safi, inayoelekea kwa vena kava ya chini ya kuendelea mpaka moyo. Damu safi ni kama asilimia 20-25 za uzalishaji wa moyo.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Figo kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.