Natiri
Mandhari
(Elekezwa kutoka Sodiamu)
Natiri (natrium; sodium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Natiri (natrium; sodium) |
Alama | Na |
Namba atomia | 11 |
Mfululizo safu | Metali alikali |
Uzani atomia | 22.98976928 |
Densiti | 0.968 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 370.87 K (97.72 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 1156 K (883 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 2.64 % |
Hali maada | imara |
Natiri (pia: sodiamu) ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 11 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 22.98976928. Alama yake ni Na. Jina latokana na chumvi asilia ya natroni alimotambuliwa. Natiri inapatikana duniani ndani ya chumvi cha kawaida cha NaCl (kloridi ya natiri) kinachopatikana kwa wingi katika maji ya bahari.
Kiini cha atomi chake kina nyutroni 11. Kuna isotopi moja tu ya kudumi ni 23Na. Peke yake ni metali laini nyeupe inayotunzwa katika mafuta kwa sababu inameyuka haraka.
-
Natiri tupu hutunzwa ndani ya mafuta ili kuzuia kumenyuka kwake
-
Moto inabadilishwa rangi na Natiri
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Natiri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |