Nenda kwa yaliyomo

Mfumo radidia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Henry Moseley (1887–1915) Mkemia

Mfumo radidia (pia: jedwali la elementi, en:Periodic table of elements) ni mpangilio wa elementi za kikemia kufuatana na namba atomia. Mpangilio huanza na namba ndogo. Namba atomia yatokana na idadi ya protoni katika kiini cha atomi.

Elementi hupangwa kwa radidi (periodi) na makundi.

Kuna radidi 7 zinazoonekana kama mstari wa kulala katika mpangilio huo. Kati ya radidi saba radidi na. 1 ina elementi mbili tu yaani hidrojeni na heli. Radidi na. 2 na radidi na. 3 zote zina elementi 8, kuna pia radidi kubwa zaidi.

Makundi yaonekana katika nguzo za kusimama. Kuna makundi 18. Elementi ndani ya kundi moja zina idadi sawa za elektroni za nje yaani kwenye mzingo elektroni wa nje. Kwa hiyo tabia zao zinafanana kikemia. Kwa mfano, kundi la 18 launganisha gesi zisizoathiri elementi nyingine kama vile heli, zenoni na arigoni.

Mfumo radidia ilianzishwa na wanakemia wawili mnamo mwaka 1869, ingawa Mrusi Dimitri Mendeleev (1834-1907) na Mjerumani Julius Lothar Meyer (19 Agosti 1830 - 11 Aprili 1895) walifanya kazi kila mmoja peke yake.

Mfumo radidia wa elementi

[hariri | hariri chanzo]
Kundi → 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18
Radidi ↓
1 1
H

2
He
2 3
Li
4
Be

5
B
6
C
7
N
8
O
9
F
10
Ne
3 11
Na
12
Mg

13
Al
14
Si
15
P
16
S
17
Cl
18
Ar
4 19
K
20
Ca
21
Sc
22
Ti
23
V
24
Cr
25
Mn
26
Fe
27
Co
28
Ni
29
Cu
30
Zn
31
Ga
32
Ge
33
As
34
Se
35
Br
36
Kr
5 37
Rb
38
Sr
39
Y
40
Zr
41
Nb
42
Mo
43
Tc
44
Ru
45
Rh
46
Pd
47
Ag
48
Cd
49
In
50
Sn
51
Sb
52
Te
53
I
54
Xe
6 55
Cs
56
Ba
*
72
Hf
73
Ta
74
W
75
Re
76
Os
77
Ir
78
Pt
79
Au
80
Hg
81
Tl
82
Pb
83
Bi
84
Po
85
At
86
Rn
7 87
 Fr
88
Ra
**
104
Rf
105
Db
106
Sg
107
Bh
108
Hs
109
Mt
110
Ds
111
Rg
112
Cn
113
Nh
114
Fl
115
Mc
116
Lv
117
Ts
118
Og

* Lanthanidi 57
La
58
Ce
59
Pr
60
Nd
61
Pm
62
Sm
63
Eu
64
Gd
65
Tb
66
Di
67
Ho
68
Er
69
Tm
70
Yb
71
Lu
** Aktinidi 89
Ac
90
Th
91
Pa
92
U
93
Np
94
Pu
95
Am
96
Cm
97
Bk
98
Cf
99
Es
100
Fm
101
Md
102
No
103
Lr
Dmitri Mendeleev (1834–1907) Mkemia

Unururifu

  • Elementi ndani ya mistari kamili zina isotopi thabiti
  • Elementi ndani ya mistari iliyovunjika zapatikana kama isotopi nururishi tu
  • Elementi ndani ya mistari ya nukta hazipatikani kiasili kwa sababu kiwango cha unururifu ni kubwa kiasi hazidumu hivyo zatengenezwa kwa mitambo (Elementi sintetiki)
  • Elementi bila mistari hazikupatikana bado zimekadiriwa tu.

Mfululizo safu wa kikemia katika mfumo radidia

Tovuti za nje

[hariri | hariri chanzo]