Fermi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fermi (Fermium) ni elementi sintetiki yenye alama Fm na namba atomia 100. Katika jedwali la elementi hupangwa katika kundi la aktinidi. Kati ya elementi sintetiki ni elementi nzito zaidi, inaweza kupatikana kwa njia ya kufyatulia nyutroni dhidi ya elementi nyepesi. Ni elementi ya kimetali ingawa metali safi ya Fermi haijatengenezwa bado. [1] Kwa jumla kuna isotopi zake 19 zinazojulikana, ikiwa 257Fm ni isotopi yenye nusumaisha ndefu zaidi iliyo na siku 100.5. Kwa sababu ya kiwango kidogo cha fermi iliyozalishwa na nusumaisha fupi ya isotopi zake zote, kwa sasa hakuna matumizi yoyote nje ya utafiti wa msingi wa kisayansi.

Fermi iligunduliwa katika taka ya mlipuko wa bomu la hidrojeni la kwanza mnamo 1952.[2] Ilipokea jina lake kwa kumbukumbu ya Enrico Fermi, mmoja wa waanzilishi wa fizikia ya nyuklia.

Fermium ilionekana kwa mara ya kwanza katika majaribio ya nyuklia ya Ivy Mike.
Elementi hiyo ilipewa jina la Enrico Fermi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Silva, Robert J. (2006). "Fermium, Mendelevium, Nobelium, and Lawrencium". In Morss, Lester R.; Edelstein, Norman M.; Fuger, Jean. The Chemistry of the Actinide and Transactinide Elements 3 (3rd ed.). Dordrecht: Springer. pp. 1621–1651. ISBN 978-1-4020-3555-5. doi:10.1007/1-4020-3598-5_13. Archived from the original on 2010-07-17. 
  2. Einsteinium. Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-10-26. Iliwekwa mnamo 2007-12-07.

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  • Fermium katika Jedwali La Purela la Video (Chuo Kikuu cha Nottingham)
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fermi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.