Nenda kwa yaliyomo

Nusumaisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majaribio ya Nusumaisha kwa kutumia kete

Nusumaisha (kwa Kiingereza: half-life) ni istilahi ya fizikia inayotaja muda unaohitajika kwa kiasi cha atomu za dutu nururifu kupungua kwa asilimia hamsini.

Elementi nururifu huwa na atomu ambazo viini si thabiti kwa sababu protoni na nyutroni huelekea kuachana. Hivyo viini hivyo vinazidi kubadilika na kuwa elementi tofauti kabisa. Katika mchakato huo unaoitwa mbunguo nururifu vinatoa chembe nururifu kama za alfa, beta au gamma.

Mfano atomu nururifu ya Kaboni-14 inatoa chembe ya beta na kuwa atomu ya nitrojeni-14.

Kama mfano wa mwatuko nyuklia, atomu ya fermi-256 inaweza kugawanyika kwa atomu mbili za xenoni-140 na palladi-112 ikiachana na nyutroni nne.

Urani-232 huwa na nusumaisha ya miaka 69. Plutoni-238 ina nusumaisha ya miaka 88, lakini isotopi ya Plutoni-242 ina nusumaisha ya miaka 375,000. Kaboni-14 inayotumiwa kugundua umri wa visukuku ina nusumaisha ya miaka 5,730.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nusumaisha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.