Nenda kwa yaliyomo

Curi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Curi (curium - pia Kuri)
Marie Curie aliyeheshimiwa kwa jina
Marie Curie aliyeheshimiwa kwa jina
Jina la Elementi Curi (curium - pia Kuri)
Alama Cm
Namba atomia 96
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 247
Valensi 2, 8, 18, 32, 25, 9, 2
Densiti 13.51  g·cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 1613 K (1340 °C)
Kiwango cha kuchemka 3383 K (3110 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0-17 %
Hali maada mango

Curi ni elementi katika mfumo radidia yenye alama Cm. Namba atomia ni 96 na uzani atomia ni 247. Ni metali nururifu ngumu sana inayohesabiwa kati ya elementi ya tamburania. Rangi yake ni kifedha-nyeupe. Ina fuwele za pembe sita.

Curi iligunduliwa mwaka 1944 na wanasayansi Wamarekani waliofanya utafiti kwa mradi wa bomu ya nyuklia. Ilipatikana kutokana na majaribio ya plutoni.

Jina limechaguliwa kwa heshima ya Marie Curie na Pierre Curie.

Curi inatoa mnururisho mkali wa chembe alfa lakini inakosa chembe gamma. Matumizi yake ni katika beteri za pekee kwa mfano beteri za vifaa vya kurekebisha pigo la moyo. Beteri inayotumia nishati nururifu inadumu muda mrefu lakini ni muhimu kuepukana na chembe gamma hatari; chembe alfa haziharibu mwili wa kibinadamu.

Elementi inatumiwa pia kwa kutengeneza tamburania nzito zaidi.


Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Curi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.