Hali maada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Maji katika hali mango ni barafu au theluji
Maji katika hali kiowevu jinsi tunavyoyajua kila siku: majimaji (isipokuwa mlimani huko nyuma ni mango)
Mvuke ya maji hauonekani lakini ni kile kinachojaza mapovu ndani ya maji yanayochemka


Hali ya maada ni muundo jinsi maada hutokea katika hali mbalimbali, ama kama elementi (dutu tupu) au kama kampaundi (dutu za mchanganyiko). Duniani kwa kawaida kuna hali tatu ya maada:

  • Hali ya nne ni utegili (plasma) lakini duniani inatokea tu katika maabara penye joto, baridi au shindikizo kubwa sana. Lakini katika ulimwengu kwa jumla maada nyingi iko katika hali ya utegili kwa sababu atomu za jua na maada ya nyota ziko katika hali ya utegili kutokana na joto kali na shindikizo kubwa.

Hali za maada hutofautiana jinsi vipande vidogo ndani ya dutu yaani atomu au molekuli zake zahusiana.

Katika hali mango zakaa pamoja kila atomu mahali pake. Tunasema: Dutu ni imara. Dutu katika hali hii ina umbo, mjao na uzani maalumu.

Katika hali kiowevu atomu zina nafasi ya kuachana na kubadilishana mahali. Twasema dutu ni kama majimaji. Dutu katika hali hii ina mjao na uzani maalumu lakini haina umbo. Kiowevu chakubali kila umbo la chombo kinamomwagwa.

Katika hali ya gesi atomu hazishikwi pamoja, zaelea kwa mwendo huria. Atomu na molekuli za gesi huelekea kusambaa na kukalia nafasi yote ambamo zimewekwa. Dutu katika hali hii ina uzani lakini haina umbo wala mjao kamili.

Atomu katika hali maada mbalimbali[hariri | hariri chanzo]