Barafu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Maporomoko ya mto mdogo yaliyoganda mlimani

Barafu ni maji yaliyoganda. Maji huganda yakishikwa na baridi na kufikia 0 °C. Barafu inaeleweka ni maji ya mgando. Hata kiowevu kingine kinaweza kushika baridi na kuganda kuwa barafu ila kama maziwa inaganda tunayaita "barafu ya maziwa".

Siwa barafu katika Atlantiki ya Kaskazini

Inapatikana katika hali na ukubwa mbalimbali. Kama ni ndogo ni fuweli kadhaa tu; kubwa zaidi ni vipande vya mvua mawe. Barafu inaweza kuwa ganda kubwa kama bapa nene sana kama lile linalofunika bara ya Antaktiki.

Barafu ina kazi muhimu katika hali ya hewa duniani. Hasa maganda ya barafu kwenye ncha za dunia yanatunza sehemu kubwa ya maji matamu yaliyopo.

Maji hupanuka yakiganda. Hivyo barafu yake inahitaji nafasi kubwa kuliko maji ya kiowevo kiasi cha 9%. Mfano wake ni chupa cha soda katika friji kinaweza kupasuka. Sababu yake ni maji ndani ya soda inahitaji nafasi kubwa kuliko soda ya majimaji hivyo kupasua chupa chenyewe.

Kutokana na hali hiyohiyo barafu ni nyepesi kuliko maji hivyo hubaki juu ya maji. Vipande vikubwa vya barafu vikivujika na barafu la Antaktiki au Aktiki vinalea baharini kama siwa barafu vinaweza kuharibu hata meli kubwa jinsi ilivyoonyesha mfano wa meli Titanic.

Kwenye mtelemko wa milima barafu yanaweza kutambaa kama mto ikiitwa barafuto.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barafu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.