Bara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Amerika Ulaya Asia Australia Australia Afrika AntaktikaContinentes.png
Ramani ya dunia inayoonyesha mabara
saba yanayohesabiwa kwa kawaida.

Bara (au kontinenti) ni sehemu kubwa ya dunia iliyochomoza juu ya bahari, ambayo kikawaida hukaliwa na watu na kuwa juu yake milima na mimea na wanyama na kila aina ya viumbe. Sehemu hii ya dunia ndio inayojulikana kama bara, na sehemu nyingine ya dunia ni ile iliyoko chini ya bahari.

Idadi ya mabara

Kwa kawaida duniani huhesabiwa mabara saba, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo.

 1. Bara la Afrika
 2. Bara la Asia
 3. Bara la Amerika ya Kaskazini
 4. Bara la Amerika ya Kusini
 5. Bara la Antaktika
 6. Bara la Ulaya
 7. Bara la Australia

Mara nyingi visiwa vya Pasifiki hujumlisha pamoja na Australia kama

na kuhesabiwa kama bara.

Kuna mahesabu tofauti yanayojumuisha Amerika ya Kaskazini na Amerika Kusini kuwa bara moja, au kinyume chake Amerika ya Kati hutazamiwa pekee. Ulaya na Asia hutazamiwa pia kuwa bara moja la Eurasia.

Mabara katika historia ya dunia

Picha ya dunia ikionyesha kutokea kwa mabara kutoka kugawanyika kwa Pangea mpaka hivi leo.

Mabara jinsi yalivyo leo hayakuwepo tangu mwanzo wala hayakai vile. Ilhali kila bara inalingana na bamba 1 au mabamba ya gandunia ina pia mwendo pamoja na bamba lake. Wanajiolojia huamini ya kwamba miaka mamilioni iliyopita mabara yote yaliwahi kukaa pamoja kama bara 1 kubwa sana lililoendelea kupasuliwa baadaye. Vipande huelea juu ya koti ya dunia ambayo ni kiowevo na moto. Mwendo wa mabamba umepimiwa kuwa sentimita kadhaa kila mwake. Uhindi zamani haikuwepo sehemu ya Asia, na sasa hivi Afrika inaelekea kupasuliwa kwenye mstari wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Eneo la Mabara ya Dunia

Bara Eneo (km²) Asilimia ya
nchi kavu yote
Wakazi
2008
Asilimia ya
Wakazi wa dunia
Msongamano
wa watu
kwa km²
Asia 43,820,000 29.5% 369,000,000 36% 86.70
Africa 30,370,000 20.4% 222,011,000 22% 29.30
Amerika Kaskazini 24,490,000 16.5% 168,720,000 16% 21.0
Amerika Kusini 17,840,000 12.0% 152,000,000 15% 20.8
Antaktika 13,720,000 9.2% 1,000 0.00002% 0.00007
Ulaya 10,180,000 6.8% 203,000,000 20% 69.7
Australia 9,008,500 5.9% 32,000,000 0.3% 3.6

Eneo la dunia

Eneo la dunia yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu.

Jiolojia ya mabara

Mabara jinsi yanavyoonekana hukaa juu ya mabamba ya gandunia ambayo ni vipande vikubwa vya mwamba vinavyounda uso wa dunia. Mabara tunavyoyajua yanalingana kila moja na bamba lake na kila bamba ina mwendo wake wa polepole. Hii ni sababu ya kwamba baada ya miaka mingi uso wa dunia utaonekana tofauti kuliko leo.

Kijiolojia bara haliishi kwenye pwani pale bahari inapoanza. Bara linaendelea chini ya uso wa bahari kama tako la bara.

Mabara na mabamba yao ni kama ifuatayo: Afrika (Bamba la Afrika), Antaktika (Bamba la Antaktika), Australia (Bamba la Australia), Ulaya na sehemu kubwa ya Asia (Bamba la Ulaya-Asia), Amerika Kaskazini pamoja na Siberia (Bamba la Amerika ya Kaskazini) na Amerika Kusini (Bamba la Amerika ya Kusini). Mabamba madogo yamejitenga ingawa nchi juu yao inaonekana kuwa sehemu ya bara lingine. Mfano wake ni Bara Hindi iliyokuwa kama bara ndogo au kisiwa kikubwa zamani lakini tangu miaka milioni 10 imejisukuma chini ya bamba la Asia-Ulaya na kuikunja hadi kutokea kwa milima ya Himalaya.

Kwa jumla miamba ya sehemu za mabara ni mipesi kushinda miamba ya chini na hii ni sababu ziko juu ya miamba mingine.

Nchi za Mabara haya

 1. Bara la Asia lina nchi huru 44.
 2. Bara la Afrika lina nchi huru 53.
 3. Bara la Amerika ya kaskazini lina nchi huru 35.
 4. Bara la Antaktika halina wakazi wa kudumu wala nchi huru hata moja ijapokuwa nchi kama 7 zinadai kumiliki sehemu fulani za bara hili.
 5. Bara la Australia au Oshania lina nchi huru 14.
 6. Bara la Ulaya (au Uropa) lina nchi huru 46.

Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi.